1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano mapya Hong Kong kupinga uhamishwaji wa wahalifu

Sekione Kitojo
14 Julai 2019

Polisi na waandamanaji walipambana tena Hong Kong Jumapili(14.07.2019) wakati machafuko yaliyosababishwa na mpango unaopingwa wa kuruhusu kupelekwa China Bara wahalifu mjini Hong Kong kuonesha ishara ya kutomalizika.

https://p.dw.com/p/3M3kl
Proteste gegen chinesische Regierung in Hongkong
Picha: Getty Images/A. Kwan

Polisi walitumia maji yenye  pilipili  na  virungu  dhidi  ya  makundi madogo  ya  waandamanaji ambao  walizuwia  barabara  pembezoni mwa  mkutano  mkubwa  mwingine  katika  eneo  la  Sha Tin , wilaya ambayo  iko  kati  ya  eneo  kuu  la  mji  karibu  na  bandari  pamoja na  mpaka  na  China.

Hong Kong | Proteste in Sha Tin
Waandamanaji katika mitaa ya Sha Tin mjini Hong KongPicha: Getty Images/AFP/P. Fong

Waandamanaji  waliofunika nyuso  zao  walijibu kwa  kuweka vizuwizi  kutokana  na  uzio  wa  chuma  na mpambano  na  polisi  wa kuzuwia  ghasia  ukaanza.

Hong Kong imetikiswa na  zaidi  ya  mwezi  mmoja  wa  maandamano ambayo  kwa  kiasi  kikubwa  yalikuwa  ya  amani, pamoja  na  wimbi la  mapabiliano  tofauti  ya  ghasia  na  polisi, yaliyozushwa  na sheria  ambayo  ingeruhusu watu  kupelekwa  China  bara  na  nchi nyingine.

Mwezi  uliopita, jengo  la bunge lilivurugwa  na  mamia  ya  watu waliojifunika  nyuso  zao,  waandamanaji  walioongozwa  na  vijana katika  tukio  ambalo  halikutarajiwa.

Mswada huo tayari umesitishwa, lakini  hatua  hiyo  haikuweza kuzima  hasira  ya  watu  ambayo  imegeuka  kuwa  vuguvugu  pana kwa  ajili  ya  mageuzi  ya  kidekrasia, haki ya kupuga kura na kuzuwia kuporomoka  kwa  uhuru  katika mji  huo wenye mamlaka yake  ya  ndani.

Proteste gegen chinesische Regierung in Hongkong
Mamia ya waandamanaji katika mitaa ya Sha Tin mjini Hong KongPicha: Getty Images/A. Kwan

Waandamanaji  pia  wanadai  mswada  huo  uondolewe kabisa , uchunguzi  huru ufanyike  kuhusiana  na  polisi  kutumia mabomu  ya kutoa  machozi na  risasi  za  mipira , wale  waliokamatwa wapewe msamaha, na  kiongozi  ambaye  hakuchaguliwa  wa  mji  huo Carrie Lam ajiuzulu.

Mamia  kwa  maelfu ya  waandamanaji  waliandamana  kupitia  mtaa wa Sha Tin leo Jumapili(14.07.2019), ikiwa  ni  wiki  ya  tano mfululizo ambayo Hong Kong imeshuhudia  maandamano  kama hayo.

Maandamano ya ghasia

Karibu  maandamano  yote yamemalizika  kwa  ghasia  kati  ya polisi  na  baadhi  ya  waandamanaji  wachache ambao wamekuwapo wakati  wote.

Hong Kong | Proteste in Sheung Shui
Polisi wakipambana na waandamanaji wakiwamwagia maji ya pilipili na kuwapiga virunguPicha: Getty Images/C. McGrath

"Tumeandamana mara  nyingi  sana  lakini  serikali  bado haitusikilizi, na kulazimisha  kila  mmoja  kuingia  mitaani," Tony Wong , mwandamanaji  mwenye  umri  wa  miaka  24  katika maandamano  hayo  ya  Sha Tin  amelieleza  shirika  la  bahari  la AFP.

Waandamanaji  wengi  wanayaona  maandamano  hayo  kama sehemu  ya  mapambano  ya  uhai  wao  dhidi  ya  kile kinachoelezwa  kama  kuongezeka  kwa  mabavu  ya  serikali  ya China.

"Huu ni wakati hatari. Watu wa Hong Kong  wanaweza  kuchagua kufa  ama  wanaweza  kuishi. Tuko ukingoni lakini  kwa  bahati mbaya  hatukufa hadi sasa  bado," amesema  JoJo So , mwanamke akiwa  katika  umri  wa  miaka  ya 50 ambaye  alihudhuria maandamano  hayo.

Hong Kong | Proteste in Sheung Shui
Makabiliano baina ya waandamanaji na polisiPicha: Getty Images/C. McGrath

Beijing imeendelea  kumuunga  mkono kwa  dhati Lam, wakiitaka polisi  ya  Hong Kong kumshughulikia  kila  mtu  anayehusika  katika kuvamia  bunge  na  mapambano  mengine.

Chini  ya  makubaliano  ya  makabidhiano  ya  mwaka  1997 na Uingereza , China  iliahidi  kuiruhusu Hong Kong  kuendelea  na uhuru wake  kama  mahakama  huru na  haki kama uhuru  wa  kutoa maoni.