1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maonyesho ya kimataifa ya Utalii mjini Berlin, Ujerumani.

7 Machi 2007

Maonyesho ya 41 ya utalii duniani yamefungua milango yake leo kwa watazamaji. Kuna vibanda 11000 katika maonyesho hayo vikiwakilisha nchi 184 na kuonesha mitindo mbali mbali ya biashara ya utalii. Mwaka huu umuhimu umewekwa katika majadiliano yanayopata kasi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Ulinzi wa hali ya hewa na utalii sio vitu vinavopingana, amesema waziri wa uchumi wa Ujerumani, Michael Glos, wakati alipoyafungua maonyesho hayo. Kwa vile uchumi unaimarika, sekta ya utalii inaweza kuwa na matumaini.

https://p.dw.com/p/CHIl
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akiyatembelea Maonyesho ya Kimatifa ya Utalii, mjini Berlin.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akiyatembelea Maonyesho ya Kimatifa ya Utalii, mjini Berlin.Picha: AP

Kuna ishara kwamba Wajerumani watabaki wakiongoza kama watu wenye kusafiri kwa wingi sana hapa duniani.

Maonesho haya yakisambaa katika kumbi kubwa 26 yatakuwa wazi hadi ijumaa kwa wafanya biashara na mwishoni mwa wiki yatakuwa wazi kwa watu wote. Vibanda vinavovutia ni vile vya kutokea Afrika, Asia na vya nchi za eneo la Bahari ya Karibian. Watu wanavutiwa wafanye safari katika Jangwa la sahara, kuendesha baskeli katika eneo la Milima ya Himlaya au kufanya likizo ya kuogolea baharini katika Bahari ya Karibian. Lakini kuna maoni mengine, kinyume na hayo. Tangazo moja linasema hivi:

+Ujerumani ni nchi nzuri kabisa kuitembelea. Jambo hilo linajulikana na kila mmoja ambaye anaitembelea nchi hii au aliye mgeni katika nchi hii.+

Wajerumani wanapenda sana kuitembelea na kufanya likizo katika nchi yao. Kila Mjerumani watatu anatumia likizo kwa kupumzika katika Milima ya Alps, ile ya katikati ya hapa Ujerumani au katika Bahari ya Kaskazini na ile ya Mashariki.

+Ile hamu ya kutaka kuota juwa haivunjiki. Lakini cha kuamua sana ni bei na huduma inayotolewa.+

Hayo yamesemwa na rais wa biashara ya utalii hapa Ujerumani, Klaus Laepple. Katika jambo hilo, Ujerumani haiko katika nafasi mbaya. Jambo hilo linawatatiza wenye kuandaa safari ngambo na wakala za safari. Kwa miongo Wajerumani wamekuwa wakiridhika kufanya ziara ya wiki mbili katika Bahari ya Mediterrenean, bei ikiingiza nauli ya ndege na usafiri hadi hotelini. Wakala za safari hutafuta nafasi kwa watalii na hujipatia bahashishi kwa huduma hiyo. Hivyo ndivyo ilivokuwa na imebakia hivyo hadi sasa. Lakini wateja maisha kilio chao ni kulitafuta juwa, ufukwe wa bahari, lakini wanaomba mambo hayo wapatiwe kwa bei nafuu.

+ Kuna mwenedno sasa ulio wazi kwamba sehemu kubwa ya ukuwaji haiko katika ile sekta ya desturi, kama vile kupitia wakala za safari, lakini watu hutumia njia nyingine, kama vile Internet na vipindi vya televisheni kuandaa likizo zao, yakiwemo pia maduka ya biashara za kawaida.+

Naam kama vile maduka ya Lidl, Aldi au Tschib o. Ikiwa ni kwenda Bahari ya Mashariki au Arabuni, Malente au Mallorca, bei zote za kusafiri hadi huko mtu anaweza kupata na kuzilinganisha kupitia Internet. Watu wengi siku hizi hujitafutia nafasi za kutumia likizo zao huko Spain, Italy na kwengine kupitia Internet. Wanatafuta wapi watapata nauli rahisi za ndege, bei nafuu za hoteli na wapi wataweza kukodi gari kwa bei ya chini. Yote ni kutaka kutotumia fedha nyingi.

Wakati mmoja kulikuweko wakala za safari 20,000 hapa Ujerumani, sasa ziko 12,000 na zinazidi kupungua. Lakini kusiweko wasiwasi kuhusu ushauri mzuri wa wakala hizo. Ujerumani kuna wakala za safari zaidi kwa kila mkaazi kuliko mahala popote pengine duniani.

Mwaka huu Indian ndio nchi rasmi shirika katika maonyesho haya ya utalii ya Berlin, ikipigiwa upatu sehemu ya Sikkim ilioko mashariki ya Milima ya Himalaya. Eneo hilo lenye mazingira mazuri ni tulivu na linaonesha vipi ulinzi wa mazingira sio kikwazo kwa maendeleo ya nchi zinazoinukia.