Nchini Tanzania baada ya kutolewa kwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichele kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ikionyesha ubadhirifu, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka, watu bado wanaizungumzia ripoti hiyo. Miongoni mwa hoja zinazotolewa ni kuwa juhudi za kuupiga vita ufisadi wakati wa utawala wa hayati rais John Pombe Magufuli ziliambulia patupu.