1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lazima kuuondoa mzizi wa tatizo

Admin.WagnerD15 Septemba 2015

Wahariri wa magazeti wanaitaka jumuiya ya kimataifa ichukue hatua ili kuing'oa mizizi ya tatizo la ukimbizi. Na pia wanatoa maoni juu ya kadhia iliyotokea nchini Misri ambako watalii kadhaa wameuliwa kwa bahati mbaya

https://p.dw.com/p/1GWlP
Wakimbizi nchini Uturuki na Ugiriki
Wakimbizi nchini Uturuki na UgirikiPicha: Reuters/O. Orsal

Gazeti la "Die Welt" linatilia maanani kwamba Ujerumani pekee inatarajia kuwapokea wakimbizi 800,000 kama siyo 1,000,000 kwa mujibu wa alivyosema Makamu wa Kansela Sigmar Gabriel.

Mhariri wa gazeti la "Die Welt" pia anakumbusha kwamba wapo wakimbizi 120, 000 wanaosubiri kugawanywa miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.Lakini mhariri huyo anasema njia ya ufanisi ya kuutatua mgogoro wa wakimbizi ni kuing'oa mizizi inayosababisha ukimbizi.


Na mhariri wa gazeti la "Sächsiche" anawaambia viongozi wa Ulaya kwamba waache kujidanganya juu ya suala la wakimbizi.Anasema kufunga mipaka siyo jawabu. Mhariri huyo anaeleza kuifunga mipaka , na kujenga kuta ndefu siyo njia ya kuwazuia maalfu wa wakimbizi wanaokuja barani Ulaya.

Migogoro lazima itatuliwe

Njia ya ufanisi ya kulitaua tatizo hilo ni kuutatua mgogoro wa nchini Syria na migogoro mingine iliyopo katika Mashariki ya Kati. Maana yake ni kwamba hata wale wanaopeleka silaha kwenye sehemu za migogoro pia wanahusika.

Mhariri anasema njia nyingine ya ufanisi ya kulitaua tatizo la wakimbizi ni kuzipa nchi masikini fursa sawa kwenye soko la dunia.

Mexico na Misri zazozana juu ya vifo vya watalii
Mexico na Misri sasa zinazozana kidiplomasia juu ya kadhia iliyotukia nchini Misri ambako watalii kadhaa waliuliwa kwa makosa na walinzi wa usalama ikiwa pamoja na raia wawili wa Mexico. Mhariri wa gazeti la "Frankfurter Rundschau anasema Rais wa Misri Al -Sisi ametoa mwito wa kupambana na magaidi kwa uthabiti wote. Na kwa hivyo siyo jambo la ajabu kwamba polisi na wanajeshi wa Misri wanahisi kwamba wanayo mamlaka ya kufyatua risasi kwanza na kuyajua mengine baadae

.Lakini katika jangwa la Sinai risasi hizo zinawapata siyo tu magaidi wanaoitwa dola la kiislamu bali pia wanavijiji. Badala ya kuyashughulikia matukio kama hayo, Misri inajaribu kukanusha na kuwalaumu wengine.

Mwandishi:Mtullya Abdu.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman