Maoni ya wahariri.
17 Agosti 2012Gazeti la "Kolner Stadt-Anzeiger" limeandika juu ya uamuzi uliopitishwa nchini Australia wa kuchapisha picha za kutisha kwenye pakti za sigara ili kuwafanya wavutaji wa sigara waingiwe uoga. Mhariri wa gazeti hilo anasema uamuzi wa kuchapisha picha za kutisha kwenye pakti za sigara ni mzuri lakini anauliza jee ni sigara tu ambazo ni za hatari kwa afya ya mwanadamu?
Na anasema Swali la msingi la kuuliza ni jee, kwa kiasi gani jamii inaweza kuwapa watu uhuru wa kuamua wanayotaka kuyafanya?Jee mwanzo wake uko wapi na mwisho wake uko wapi? Jee pia haitakuwa sahihi pia kuchapisha picha za kutisha kwenye chupa za mivinyo,bia na pombe kali ili kuwatahadharisha watumizi juu ya hatari.Lakini mtu akifikiri zaidi atatambua kwamba jamii inayojaribu kuwalinda watu wake kwa njia hiyo pia inageuka kuwa ya udikteta wa kijamii.
Mhariri wa "Neue Presse" anakubliana na hoja hiyo na anaeleza kwamba hatua iliyochukuliwa nchini Australia inalenga shabaha ya kuwatisha wavutaji wa sigara ili wasiwe na hamu tena na tumbaku . Mhariri anasena huenda hatua kama hiyo ikachukuliwa katika nchi za Ulaya vile vile.Lakini, jee utekelezaji wa umauzi huo siyo udikteta wa kijamii? Pamoja na hayo, anaetaka kuchukua hatua kali dhidi ya sigara anapaswa pia kuchukua hatua kali dhidi ya pombe. Itampasa aonyeshe picha za ini la mtu lililolika kabisa. Mhariri anauliza, jee tunayataka hayo?
Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linatoa maoni juu ya mkataba mpya uliofikiwa baina ya serikali ya jimbo la Hamburg na waislamu wa jimbo hilo.Pamoja na mambo mengine mkataba huo utawapa waislamu haki sawa, juu ya siku kuu zao na mafunzo ya dini shuleni. Gazeti hilo linasema, mkataba huo mpya ni ishara tu na kwa kweli hali halisi inayowakabili Waislamu nchini Ujerumani haitabadilika kwa jumla. Wafanyakazi watakuwa na haki ya kuchukua likizo wakati wa siku kuu. Lakini hayo yatakuwa na maana ikiwa mpaka sasa waajiri walikuwa wanawakatalia.
Gazeti la "Westdeutsche" linatoa maoni juu ya uwezekano wa kupanda kwa bei za vyakula kutokana na ulanguzi kwenye masoko ya dunia. Gazeti hilo linasema walanguzi wanaitumia hali ya ukame nchini Marekani kupandisha bei. Lakini kwa kweli kiasi cha mavuno kitakachopungua ni asilimia mbili tu ya mavuno ya mwaka uliopita. Kinachoweza kusaidia ni kupiga marufuku ulanguzi wa vyakula badala ya kupiga marufuku uuzaji wa mafuta yanayotokana na mimea.
Mwandishi:Mtullya abdu/Deutsche Zeitungen/
Mhariri:Abdul-Rahman