1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz

Abdu Said Mtullya13 Februari 2014

Wahariri wanazungumzia juu ya hotuba ya Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz iliyotifua zogo nchini Israel.Pia wanatoa maoni juu ya kuupa utawala wa Obama ruhusa ya kuendelea kukopa

https://p.dw.com/p/1B7ul
Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz
Spika wa Bunge la Ulaya Martin SchulzPicha: picture-alliance/dpa/Knesset Spokesman Office/Handout

Lakini kwanza maoni ya gazeti la "Darmstädter Echo juu ya hotuba aliyoitoa Spika wa Bunge la Ulaya bwana Martin Schulz kwenye Bunge la Israel Knesset.

Katika hotuba yake Spika wa Bunge la Ulaya alizungumzia juu ya hali mbaya za maisha ya Wapalestina katika maeneo yanayodhibtiwa na Israel. Bwana Schulz alisema katika hotuba yake kwamba aliulizwa na kijana mmoja kaika Ukingo wa Magharibi kwa nini Muisraeli anaruhusiwa kutumia Cubic mita 70 za maji kwa siku wakati Mpalestina anaruhusiwa Cubic mita 17 tu.

Wabunge wa Israel wamsusia Schulz

Wabunge wa Israel wa vyama vya mrengo wa kulia walikasirika na kutoka bungeni. Juu ya kadhia hiyo mhariri wa gazeti la "Darmstädter Echo" anasema ni wazi kwamba kila Mjerumani anaehutubia kwenye Bunge la Israel anapaswa kuyakumbuka maafa yaliyowafika Wayahudi.Lakini pamoja na nadhari yote inayopaswa kuzingatiwa, kusema ukweli ni jambo la lazima.

Bwana Schultz alipewa shahada ya heshima na chuo kikuu cha Jerusalem , ya kuutambua mchango wake katika kupambana na chuki inayoelekezwa kwa Wayahudi. Kadhia ya hapo jana inaonyesha kwamba wale wanasiasa vichwa ngumu nchini Israel wanapoteza uzito wao.

Schulz alipaswa kuwa na nadhari

Katika maoni yake gazeti la "Bild" linasema Spika wa Bunge la Ujerumani alipaswa kuwa na nadhari katika ulimi wake alipohutubia kwenye Bunge la Israel.Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba ilikuwa heshima kwa Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz kuhutubia kwenye Bunge la Israel. Lakini pia ulikuwa wasaa wa kuwa mwangalifu. Hata hivyo bwana Schulz aliamua kuishambulia serikali ya Israel katika hotuba yake.

Gazeti hilo linasema kama mwakilishi wa Umoja wa Ulaya na kama Mjerumani bwana Schulz alikuwa na wajibu wa kuonyesha mshikamano na Israel.Kwa tufani aliyoitifua ,hana budi aombe radhi.

Mhariri wa gazeti la "Neue Osnabrücker " anasema ni heshima kwa mwanasiasa wa Ujerumani kutoa hotuba kwenye Bunge la Israel. Lakini pia ni changamoto.Hata hivyo, mgeni pia anastahili kusikilizwa. Anayo haki ya kuikosoa Israel.

Bajeti ya Marekani

Gazeti la"Badische Neueste Nachrichten" linatoa maoni juu ya mvutano wa bajeti nchini Marekani ambao safari hii umeepushwa mapema. Mhariri huyo anasema chama cha Republican kinachoyazingatia maadili ya biashara huru hakiwezi mara kwa mara kusababisha mkwamo wa fedha katika serikali.

Uamuzi wa haraka wa kuiruhusu serikali iendelee kukopa unaonyesha kwamba watetezi wa maadili ya biashara huru katika chama cha Republican wamechagua kuepusha maafa.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman.