1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Maoni ya Waganda kuhusu mzozo wa Israel na Hamas

11 Oktoba 2023

Mapigano kati ya kundi la Hamas na taifa la Israel yameibua maoni mseto miongoni mwa watu kwenye sehemu mbalimbali za dunia.

https://p.dw.com/p/4XPp0
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta MuseveniPicha: SNA/IMAGO

Nchini Uganda, watu wanahimiza mzozo huo kutohusishwa na hisia au itikadi za kidini kwani mtazamo huo utawafanya wengi waache kuzingatia hali halisi ya mgogoro huo ambaoumedumu kwa zaidi ya miaka 70 bila kupatikana suluhu ya kudumu.

Wengi wa watu tuliowahoji hawataki mzozo huo kutajwa kuwa vita ila mapigano kati ya kundi la magaidi ambao hawana ridhaa kutoka kwa watu wa Palestina.

Soma pia:Umoja wa Mataifa waionya Israel juu ya kuizingira Hamas

Baadhi wanapendekeza jumuiya ya kimataifa kuwezesha kuwepo kwa mataifa mawili yanayoheshimu haki za binadamu.

Uwepo wa makabiliano ya aina yoyote yatazidisha maafa ya watu ambao wanahitaji amani.

Kutokana na matamshi ya viongozi mbalimbali duniani na pia watu wanaoelezewa kuwa wenye itikadi kali za kidini.

Mitazamo ya kidini katika mzozo

Kuna dhana kwamba hisia za chuki za kidini zinahusishwa katika mgogoro huo.

Lakini baadhi ya watu nchini Uganda wanaelezea kuwa si sawa kudhani kwamba Hamas wanaungwa mkono na raia wote wa Palestina wala jumuiya ya waislamu.

Piaisichukuliwe kuwa watu wa Imani za kikrsito wataiunga mkono Israel pale inapokiuka sheria za kimataifa katika operesheni zake.

Mataifa ya A Afrika ikiwemo Uganda yanaathirika vipi na mzozo huo kwa kiwango fulani kutokana na mahusiano ya pande hizo.

Baadhi ya waafrika wapo matika nchi kama Israel ikiwemo masomo na sababu zingine za kibiashara na kijamii.

Soma pia:Ni lipi kusudio la Hamas kuwachukua mateka raia wa Israel?

Kile ambacho watu wote wanakubaliana nacho ni kwamba viongozi kote duniani wana uwezo wa kukomesha mzozo wa Palestina na Israel.

Baadhi ya wafuatiliaji wanaamini kuwa viongozi wa dunia watafanikiwa ikiwa hawataweka maslahi binafsi ila maslahi jumuishi ya jamii ya kimataifa kuhakikisha amani na uthabiti katika eneo hilo lililoshuhudia mizozo kwa mikongo kadhaa. 
 

Israel kuuzingira Ukanda wa Gaza