1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni : Vituo ya kushikilia wakimbizi nchini Misri?

3 Machi 2017

Kwa mujhibu wa viongozi wa Misri na Unjerumani suala la vituo vya kuwashikilia wakimbizi haliko katika agenda angalau kwa hivi sasa lakini suala hilo haliondoki anaandika mwandishi wa DW Dagmar Engel katika maoni yake.

https://p.dw.com/p/2YaPD
Ägypten Angela Merkel & Abdel Fattah-al-Sisi
Picha: picture-alliance/Anadolu Agency/Egyptian Presidency

Kwa kawaida sera ya kigeni haifuati mpango wa kufanya ziara ya taifa,kufunga mikataba na kuondoka.Juu ya kwamba yumkini kukawa na baadhi ya marais wangelipenda kuamini hivyo lakini kwa hakika rais wa Misri sio miongoni mwao. Licha ya yeye na serikali yake matatizo kuwafikia shingoni ..........uchumi wa nchi uko katika hali mbaya ,theluthi ya wananchi wa nchi hiyo wanaishi chini ya kiwango cha ufukara na hali ya kuroridhika na maiasha imekuwa ikizidi kuongezeka.

Lakini licha ya hayo Misri bado inaonekana kuwa nanga ya utulivu katika kanda hiyo.Na al-Sisi anajuwa kwamba sio Kansela wa Ujerumani au Waziri Mkuu wa Israel au Rais wa Urusi au kanda hiyo nzima bali dunia nzima kwa jumla watakubaliana na mambo kuendelea kuiweka nchi hiyo katika hali hiyo. Yumkini wakakubaliana juu ya baadhi ya mambo lakini tutarajie sio kila jambo.Ni jambo lisilokanushika kwamba wakimbizi na wahamiaji wengine pia nchini Misri wanaishi katika mazingira yanayopaswa kuboreshwa.  Ni suala lisililokuwa na ubishi kwamba watu wanaowasafirisha binaadamu kwa magendo lazima wazuiliwe au angalau shughuli zao zikwamishwe kwa njia fulani.

Msaada na kinga

Kommentarbild Kommentatorenfoto Dagmar Engel
Mwandishi wa DW Dagmar Engel.

Inaonekana ni jambo sahihi na sawa kwamba Misri inapaswa kuwapokea watafuta hifadhi wanaorudishwa baada kukataliwa maombi yao ya hifadhi.Kuanzisha uwezekano wa kisheria kuja Ulaya linaonekana ni jambo zuri.Kutowa fedha kuzalisha ajira hii penine inaweza kuwa silaha muafaka kabisa ya kupambana na sababu kuu inayopelekea watu kukimbia.Yote hayo yanaonekana hatua inayofaa ya kinga.Bado hakuna Wamisri wengi wanaotaka kuondoka katika nchi yao kuelekea Ulaya na pengine hali hiyo itaendelea kubakia hivyo.

Suala liliopo kipi kitakachokubalika na gharama gani zitakubaliwa kulipwa. Je itaruhusiwa kuliunga mkono taifa hilo lenye kutumia ukatili wa polisi na rais mwenye kutawala kwa mabavu kulilea kiuchumi kwa sababu tu mfumo huo unaahidi utulivu?  Gharama gani zinastahiki kuzuwiya machafuko ya Libya yasienee kuingia Afrika kaskazini nzima ? Tuko tayari kwa kiasi gani kuwekeza kuzuwiya Urusi na China kuwa na ushawishi mkubwa kabisa kwa kanda hiyo? Kinahitajika kiasi gani kuifanya Misri ianzishe vituo vya kushikilia wahamiaji pengine sio sasa lakini baadae ili kwamba wasije Ulaya? Kansela Merkel amesema nchini Misri kwamba mashirika ya kiraia yaliyoendelea yana maana sana kwa maendeleo na ushuhupavu wa kupambana na ugaidi.Ni ziara ya manufaa.

Mwandishi : Dagmar Engel/Mohamed Dahman

 Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman