CDU, CSU na SPD vyaweka kando tofauti kuhusu uhamiaji
6 Novemba 2015Ni vizuri kwamba hakutakuwa na uzio wa waya ama ukuta ambao maelfu ya wakimbizi watawekwa humo katika kipindi cha mpito kabla ya kuchujwa na kuwatambua wale wakimbizi halali na wasio halali na wengine wasubiri kurejeshwa makwao.
Maeneo hayo yanayoitwa , maeneo ya muda ya mapokezi kwa wahamiaji wanaosafiri kuja Ujerumani ni wazo lililotokana na chama cha CSU cha jimboni Bavaria.
Jaribio la kuingia nchini Ujerumani bila ya uwezekano wa kubakia , lipatiwe ufumbuzi wa haraka.
Lakini kambi kama hiyo , japo haina mtazamo wa gereza la Guantanamo ama vituo vya mateso vya utawala wa Wanazi nchini Ujerumani, si tu zimeleta mvutano wa kisheria, lakini pia hazina nafasi katika wakati huu tulionao.
Mpango mbadala wa kuwahudumia wakimbizi
Pamoja na hayo chama cha CSU kiliendelea na mtazamo wake, lakini mwishoni kumepatikana mwelekeo na udhibiti mzuri kwa wimbi la wakimbizi wanaoingia katika jimbo la Bavaria.
Kinyume na vituo vya kuwapokea wakimbizi kwa muda , sasa kuna mahali maalum pa kuwapokea wakimbizi, ambako wanaasajiliwa kwa haraka na kuthibitishwa. Wakimbizi wanaweza kutembea watakako , lakini ni lazima wasalie katika eneo walikofikia.
Hatua zote hizo ni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa maombi ya waomba hifadhi na pia kuweza kuwapatia mafao ya kijamii.
Wakimbizi wachache wanaingia
Haina maana kwamba huenda wataingia sasa wakimbizi wachache kwa kuwa na utaratibu huu , kwa kudhani kwamba watafikiri hawatatambuliwa na kupatiwa kibali cha kuishi nchini Ujerumani.
Maelfu tayari wameingia wiki zilizopita bila kusajiliwa. Muda utaonesha vipi watafanya.
Uhispania wamehalalisha tangu muongo mmoja uliopita maelfu ya watu wasiokuwa na makaratasi, na wamejumuishwa katika jamii.
Vyama vinavyounda serikali ya mseto baada ya mvutano huu , hususan mkuu wa chama cha SPD Sigmar Gabriel , walikubaliana kwa busara.
Hata hivyo vyama hivyo vinavyounda serikali vinapaswa kuangalia utendaji wa uamuzi wao, na kufikiria kuhusu wakimbizi kutoka Afghanistan kwa mfano ambao wamekuwa wakilindwa dhidi ya sheria ya kuwarejesha nyumbani.
Tunapaswa kukumbuka yale yanayoelezwa na idara ya maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani kuhusu yale tunayoyasikia kila siku kuhusu ugaidi wa kundi la Taliban. Nchini Afghanistan pekee vikosi vya jeshi la Ujerumani vimeimarisha ulinzi katika maeneo yake ili Waafghanistan wabakie nchini mwao.
Hii ni sawa na wazo lililozikwa la kuweka makambi ya kuwapokea wakimbizi nchini Ujerumani. Upinzani na mashirika ya kutoa misaada vinapaswa kupingana na hilo.
Mwandishi : Gräßler , Bernd / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Josephat Charo