Maoni: Ushindi wa Trump washtua wengi
9 Novemba 2016Bila shaka, mipango yake, nia yake, mawazo yake, maneno yake makali hisia zake za ubaguzi, maneno yake matupu yote yalionekana wakati wa kampeni za uchaguzi. Lakini katika usiku wenyewe wa uchaguzi Trump alionekana kuwa ni mtu aliyekuwa tayari kuiunganisha upya Marekani baada ya kupakwa matope na vilevile alionyesha kuwa yuko tayari kukutana na washirika wengine duniani kote. Kwa ufupi inabidi kusubiri ili kuweza kuona haya yote yakitendeka.
Hakuna mtu aliyejiandaa kwa ushindi wa Trump
Hata hivyo,Ushindi wa Trump ni habari mbaya kabisa katika serikali za Magharibi na bila shaka hata mjini Berlin. Hakuna aliyekuwa amejitayarisha juu ya ushindi wake vile vile haijulikani ni nani atakepewa jukumu la kufanya maamuzi ya mwisho katika sera za mambo ya nje, usalama, ulinzi na mazingira. Trump ni sawa na mtu wa nje ndani ya chama cha Republican, hivyo basi yeye hategemei watu wanaojulikana au wasomi. Kwa maana hiyo itazidi kuwa vigumu kwa mambo kufanyika hasa kwakuwa huenda Trump atazungukwa na watu ambao hawana ujuzi na uzoefu katika uwanja wa kisiasa.
Hali hii bila shaka inaweza kuleta athari katika sera za kiuchumi, ambazo zinategemea soko huru la biashara ya kimataifa, sera za kigeni na usalama ambazo zinahusu Iran; suala la Israeli, na pia kuhusu uwezekano wa hatua za kijeshi dhidi ya makundi yya kigaidi ya Jihadi ; na vile vile bila ya kusahaulika uhusika wa serikali ya Marekani katika swala la Mashariki ya Kati pamoja na uhusiano tete na nchi za Urusi na China;athari hizi ni pamoja na uwezo wa kutambua iwapo Marekani ni mshirika au mpinzani wa mataifa haya mawili makubwa au inataka kujitenga.
Kuhusu uhusiano na nchi washirika. Je Marekani itaendeleza ushirikiano na jumuiya ya kujihami ya NATO kwa ajili ya mfumo wa usalama wa pamoja wa nchi za Magharibi? Je Trump ana nia ya sera ya ushirikiano? Au anamini kwamba Wazungu watabidi kulipa zaidi kwa ajili ya usalama wao? Na huo ndio mtihani mkubwa kwa nchi za Magharibi.
Trump si miongoni mwa wasomi
Donald Trump si mtu anaejulikana sana. Yeye anajulikana tu kama billionaire kutoka New York – na mshindi kutoka kwenye jimbo hadi kwenye miji, yeye si miongoni mwa tabaka la wasomi au watu wanaojulikana sana kwa hiyo haitakuwa rahisi kumfikia.
Lakini mshtuko na hofu pia vina upande wake mzuri. Hadi Trump atakapo ingia katika ikulu ya Whie House mwezi Januari kama rais wa 45 wa Marekani hadi hapo atakuwa na muda wa kutosha wa kujiweka sawa. Kuchaguliwa Donald Trump ni hatua ya mageuzi, pengine hata kihistoria. Hata hivyo haina maana kuwa ndio mwisho wa ushirikiano na nchi za Magharibi kwa sababu ya wasiwasi uliopo. Lakini jambo moja la uhakika ni kwamba Trump ni mtu mwenye desturi isiyo ya kawaida.
Mwandishi Zainab Aziz/Kudascheff Alexander
Mhariri:Yusuf Saumu