1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lazima kuomba radhi

14 Julai 2016

Serikali ya Ujerumani imekubali, kwamba mauaji ya Waherero nchini Namibia yalikuwa ya kimbari. Lakini kinachotakiwa sasa ni kuomba radhi kwa kile ambacho wakoloni wa Kijerumani walikitenda kwa watu hao

https://p.dw.com/p/1JP09
Askari wa kikoloni wa Ujerumani nchini Namibia
Askari wa kikoloni wa Ujerumani nchini NamibiaPicha: picture-alliance/dpa/W. Gebert

Ilipohusu mauaji ya halaiki ya watu wa Armenia yaliyofanywa na utawala wa Osman, mnamo mwaka wa 1915 bunge la Ujerumani halikuwa na matatizo juu ya kulitumia neno hilo la mauaji ya halaiki. Labda kwa sababu suala hilo limeihusu Uturuki na kisasili juu ya kuundwa kwake.

Rais wa nchi hiyo,Erdogan alijibu kwa kusema kwamba Ujerumani inapaswa kuwa nchi ya mwisho kutoa hukumu iwapo utawala wa Osmani ulifanya mauaji ya halaiki. Erdogan amesema Ujerumani haina budi iwajibike juu ya Waherero zaidi ya laki moja walioangamizwa wakati wa ukoloni wake nchini Namibia.

Erdogan amesema kweli

Spika wa Bunge la Ujerumani Nobert Lammert amesema ni jambo la fedheha kwamba hakuna maelezo ya uwazi kutoka upande wa Ujerumani.

Mwandishi wa maoni Claus Stäcker(Mkuu wa idara ya Afrika)
Mwandishi wa maoni Claus Stäcker(Mkuu wa idara ya Afrika)Picha: DW

Shinikizo la kuyatambua mauaji ya Waherero kuwa ya halaiki liliimarika kuanzia hivi karibuni.Sababu ni kwamba neno hilo lilianza kutumika baada ya azimio la Umoja wa Mataifa juu ya kuzuia na kuadhibu uhalifu wa mauaji ya halaiki lililopitishwa mnamo mwaka wa 1951 na kwa hivyo liliondolewa kwenye msamiati wa serikali.

Kwenye shughuli ya kuyakumbuka mauaji hayo mnamo mwaka 2004 aliekuwa Waziri wa Ujerumani wa ushirikiano wa maendeleo Haidemarie Wieczorek Zeul alisema mauaji ya Waherero na Wanama yanaweza kutambuliwa kuwa ya kimbari ,katika msamiati wa leo. Waziri huyo pia aliomba radhi kwa niaba ya serikali ya Ujerumani .

Lakini kauli yake ilimgonganisha na aliekuwa Waziri wa mambo ya nje wa wakati huo Joshka Fischer aliekuwa na wasi wasi juu ya suala la kulipa fidia.

Lakini nyakati na serikali zimebadilika

Pendekezo lililotolewa na aliekuwa mbunge wa chama cha upinzani,mnamo mwaka wa 2012, Frank-Walter Steinmeier ambae leo ni Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani lilitoa mwongozo. Alisema vita vya maangamizi nchini Namibia kuanzia mwaka wa 1904 hadi 1908 vilikuwa uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari. Kauli hiyo imekuwa sera ya serikali na pia ni msingi wa mazungumzo juu ya maridhiano na fidia yanayofanyika sasa na serikali ya Namibia.

Na hivi karibuni ,mjumbe maalumu Ruprecht Polenz na mwakilishi wa Ujerumani Georg Schmidt kwa mara nyingine walikutana na wajumbe wa serikali ya Namibia mjini Windhoek. Wawakilishi hao wa Ujerumani wanataka kufikiwa makubaliano yasiyotazama nyuma bali yanayozingatia mustakabal.Mtazamo huo unaungwa mkono nchini Namibia pia.

Mazungumzo yanatazamiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwaka huu.Tamko linatarajiwa kutolewa na serikali na bunge kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini Ujerumani mwaka ujao. Ni tamko la kuomba radhi ambalo limekuwa linasubiriwa kwa muda mrefu sana na vizazi vya Waherero na Wanama walioangamizwa.

Sasa wataalamu wa historia wanajadiliana juu ya idadi ya watu waliouliwa.Huenda idadi ikawa chini ya laki moja. Uhalifu uliotendwa umeorodheshwa na inapasa fidia itolewe. Kusema tu kwamba serikali za Ujerumani zimekuwa zinatoa misaada mikubwa ya maendeleo siyo hoja tena.

Wahusika wamekuwa wanakwepa kuwajibika au aghalabu wamelitupia suala hilo kwenye ngazi za chini za serikali. Sasa suala la nani atafidiwa na kwa kiasi gani linajadiliwa.Suala hilo ni tata licha ya kuwapo nia nia njema. Suala hilo linaendelea kuchemka licha ya wawakilshi wa Ujerumani na Namibia kusisitiza mara kwa mara kwamba mazungumzo yanaendelea vizuri.

Mwandishi: Stärke Claus

Mfasiri: Mtullya Abdu

Mhariri: Mohammed Khelef