1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Tangazo la vita dhidi ya demokrasia

20 Oktoba 2016

Ulikuwa mdahalo wa mwisho kuwania urais wa Marekani kati ya Donald Trump wa chama cha Republican na Hilary Clinton wa Democrat, ambao mwandishi wa DW, Ines Pohl, anauona ni tangazo la vita dhidi ya demokrasia.

https://p.dw.com/p/2RTGC
USA | Ende der 3. Präsidentschaftsdebatte 2016 in Las Vegas
Picha: REUTERS/M. Blake

Mdahalo huo kwa usahihi na kujiamini uliendeshwa na Mann Chris Wallace wa kituo cha televisheni cha Fox. Ameonyesha kwamba ilikuwa ni sahihi kukiachia kituo hicho cha kihafidhina kuendesha mjadala wa kuwania urais kwa mara ya kwanza.

Kwa wale ambao hali ya maisha yao ni ya kusikitisha taarifa za mwisho za kuufunga mdahalo huo wa dakika tisini zilitiliwa maanani. Zilitosha kuonyesha ustahiki wa wagombea katika nafasi hiyo ya juu kabisa ya kisiasa.

Wakati Clinton kwa  kujiamini alitowa muhtasari wa ajenda yake ya kisiasa, Trump alikuwa 'akibangaiza' kutoka mada moja hadi nyengine na hakuonyesha mpango wowote wa kutimiza ahadi zake zilizojaa makuu. Anaona Clinton anaunga mkono maovu yote nchini Marekani na sehemu nyingi duniani. Kulaumu wengine kwa makosa yako ni kitu cha hatari sana.

DW Mitarbeiterin Ines Pohl
Ines Pohl mwandishi wa DW.Picha: DW

Mtu anaweza kumwelezea Trump kwa mengi lakini hawatowacha kueleza kwamba hawezi kushinda uchaguzi huu.

Kutojiandaa kwake vya kutosha kwa midahalo muhimu ya televisheni, kukiandamana na kuwadhalilisha wanachama wenzake, kunawafanya baadhi ya watu nchini Marekani waamini kwamba kwa vyoyote hataki urais huo.

Kuanzia mwanzo kabisa amesema wafuasi wa vyama vyote viwili, Democrat na Republican, walichokifanya ni kulifanya jina la Trump lizidi kuwa na thamani.

Pengine inaweza kuwa hivyo. Na ingelikuwa Trump ni mwanasiasa wa aina yake na mwenye heshima, hilo lingelikuwa ni jambo la kutafakariwa na chama cha Republican.

Lakini inakuwaje tapeli huyo anaweza kukiteka nyara chama cha Abraham Lincoln?

Trump hana heshima wala uadilifu hata mbele ya misingi ya demokrasia. Kwa wale waliopoteza imani na mfumo wa utawala wa serikali, wale wanaotumia kila fursa kusalimu amri kwa nadharia za njama na kulaumu wengine kwa makosa yao, Trump amelitumia hilo vizuri katika kampeni yake na hivi sasa anadhoofisha misingi ya demokrasia kwamba walio wengi wape.

Kwa Trump baruti ya kisiasa imeibuka ambayo inahoji mfumo wa kijamii uliopitia mtihani na kujaribiwa kwa karne nzima. Hiyo ni hatari inayokwenda mbali zaidi kuliko hata Donald Trump kama mtu.

Mwandishi: Ines Pohl/Mohamed Dahman

Mhariri: Grace Patricia Kabogo