1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yapeleka wanajeshi 5000 kuhimiza amani na utulivu DRC

Lubega Emmanuel 30 Machi 2023

Hatua ya Uganda kupeleka wanajeshi 5,000 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushiriki katika mpango wa kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo imepokelewa kwa maoni mseto na raia wa nchi zote mbili.

https://p.dw.com/p/4PWJM
Demokratische Republik Kongo | Soldaten von Uganda und DRC | Archivbild
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Kikosi cha Uganda kinajiunga na kile cha Kenya , Burundi na Sudan Kusini chini ya mpango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kuleta amani na utulivu maeneo ya Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mapigano kati ya kundi la M23 na majeshi ya Congo katika kipindi cha mwaka mmoja sasa hasa eneo la Rutshuru yaliwalazimu zaidi ya raia 70,000 wa Congo kukimbilia Uganda na kusababisha hali ya sintofahamu pale kundi hilo lililodhibiti sehemu nyeti ambako bidhaa kati ya Uganda kuelekea mji wa Goma zimekuwa zikipita.

Raia mbalimbali wa Uganda na wakimbizi kutoka Congo wana maoni mseto kuhusu mpango huo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupeleka majeshi katika nchi hiyo mwanachama wake.

Wana mtazamo kuwa majeshi hayo yataweza tu  kuwadhibiti vilivyo wapiganaji wa M23 ambao inadaiwa ndiyo chanzo cha ukosefu wa utulivu eneo hilo ikiwa watakubali kushirikiana na utawala wa Congo na kuondokana na mapambanao yao. Wanataka Pamoja na juhudi za kijeshi, kuwepo pia mazungumzo ya dhati na ya haraka kati ya kundi hilo na majeshi ya Congo ili kuleta amani ya kudumu.

Kikosi cha Sudan Kusini pia kimejiunga na wenzao wa EAC

Südsudan, Juba | Soldaten bereitet sich auf ihre Abschlussfeier vor
Wanajeshi wa Sudan Kusini Picha: Waakhe Simon Wude/DW

Kulingana na viongozi wa Bunagana, idadi ya raia wa congo wanaoingia Uganda imepungua ikilinganishwa na hapo awali ambapo walikimbilia Uganda katika makundi ya mamia.

Wakiwaaga wanajeshi hao, makamanda wa Uganda wamewataka kuzingatia  ushirikiano mwema na raia wa Congo. Kanali Michael Walaka ndiye kamanda wa kikosi cha Uganda kilichoelekea Congo chini ya mpango wa kijeshi wa Jumuiya ya afrika mashariki.

Kulingana na taarifa ya katibu mkuu wa Jumuiya ya afrika mashariki Dkt. Peter Mutuku Mathuki kikosi cha Sudan Kusini nacho kimejiunga katika mpango huo hapo jana na kuelekea eneo wanakotakiwa kuendesha juhudi za kuleta amani. Ikumbukwe kuwa kwa sasa Uganda ina vikosi viwili tofauti nchini Congo.

Kikosi kimoja kilienda mwaka 2021 kupambana na waasi wa ADF wanaotokea Uganda. Wakiwaaga wanajeshi hao, makamanda wa Uganda wamewawataka kuzingatia jukumu la kuleta amani na kushirikiana vyema na raia wa Congo. Mimi ni

Mwandishi: Lubega Emmanuel DW.