Maoni juu ya msaada wa Mabilioni kwa Mali
17 Mei 2013Washiriki mia moja pamoja na wawakilishi wa mashirika waliahidi kutoa jumla ya Euro Bilioni tatu na robo,kwa ajili ya ujenzi mpya wa Mali. Kiasi hicho cha fedha,ni sawa na Cefa Trilioni mbili za Mali. Ni ishara nzuri na pia ni nguvu kubwa kwa Mali.
Kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na kwa kweli ni zaidi ya kile ambacho mtu alikitarajia. Walioahidi kutoa msaada siyo Marekani,Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya tu. Benki ya maendeleo ya Kiislamu pia itasshiriki katika juhudi za kuijenga upya Mali.
Maslahi ya jumuiya ya kimataiafa:
Ushiriki wa pande hizo unathibitisha maslahi ya jumuiya ya kimataifa juu ya maendeleo ya Mali. Hata hivyo dunia bado inakumbuka vizuri yaliyotokea nchini Irak na Afghanistan kwamba mabilioni ya fedha peke yake hayawezi kujenga nchi ambayo mtu anaeitamani bila ya kuekezwa vizuri.
Msaada kwa ajili ya Mali ni hatua ya ujasiri ya kuekeza katika mustakabal wa nchi hiyo.Kwani ni fedha kwa ajili ya nchi ambayo kwa kweli haipo-yaani nchi ya kidemokrasia. Nchi ya Mali ambayo baada ya vita, kuangushwa kwa serikali na ujiingizaji wa kijeshi kutoka nje,itarejea katika ufahamu.
Usalama na vita dhidi ya rushwa:
Mali itapaswa kuwa nchi ya kuondoa rushwa ,nchi itakayokuwa tayari kuikaribisha dunia, nchi itakayotenganisha dini na serikali na nchi itakayokuwa ya kuaminika, imara na ya usalama.
Ni miaka 11 iliyopita tokea aliekuwa Rais wa Ujerumani Johannes Rau alipofanya ziara nchini Mali ambako aliisifu nchi hiyo kuwa mfano mzuri wa demokrasia na uhuru wa kutoa maoni barani Afrika. Mali ilitambulishwa kwa Rais huyo wakati huo kama mnara wa nuru barani Afrika, katika ngazi sawa na nchi kama Afrika Kusini,Ghana na Botswana.
Wataalamu wa Ujerumani waliilezea Mali kuwa kigezo cha mafanikio kuhusu meguezi ya kidemokrasia. Hata Spika wa Bunge la Ujerumani Nobert Lammert anaelitembelea bara la Afrika kwa nadra aliichagua Mali kuwa mahala pa kufanyi ziara. Lakini miezi michache baadae ,Mali ilianza kusambaratika.
Aghalabu wataalamu wa Ujerumani na wa Ulaya kwa jumla hufanya makosa juu ya ufafanuzi wao juu ya demokrasia barani Afrika.
Lakini Mali inapinga kusambaratika:
Ikiwa mradi wa kuioka Mali utashindikana, basi wanajihadi,na wale wanaotaka kujitenga, na wale wanaochochea vurumai wataitia nchi hiyo mikononi mwao .Mambo yakienda mrama nchini Mali, bara la Ulaya pia litakuwamo hatarini. Kwa hivyo uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika nchini Mali mnamo mwezi wa Julai utakuwa mitihani wa hali halisi
Matayarisho ya uchaguzi ni changamoto kubwa.Maalfu ya wakimbizi wa Mali wanaishi nje ya nyumbani kwao. Na jee vipi juu ya kampeni za uchaguzi.Jee zitaishia katika mji mkuu na katika sehemu ya kusini mwa nchi tu.?Na nini kitatokea kwa sehemu ya kaskazini mwa Mali yenye majimbo yasiyoitii serikali kuu .
Mchango wa Ujerumani:
Suala jingine muhimu sana ni usalama wa nchi hiyo.Jee majeshi ya Umoja wa Mataifa yanayopangwa kupelekwa Mali yatakuwa na uwezo kuchukua mahala pa majeshi jarabati ya Ufaransa?
Ujerumani inashiriki katika kuijenga upya Mali kwa mchango wa Euro zaidi ya Milioni 200.Pana matumaini juu ya Mali. Mchakato wa demokrasia ulioanza mnamo mwaka wa 1991 pia ultanguliwa na serikali kuangushwa.
Mwandishi: Claus Stäcker
Tafsiri:Mtullya Abdu.
Mhariri:Abdul-Rahman