1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni juu ya mkutano wa viongozi wa Afrika na wa Ulaya

Abdu Said Mtullya3 Aprili 2014

Mkutano wa kilele baina ya viongozi wa Afrika na wa Umoja wa Ulaya umemalizika mjini Brussels.Pamoja na mambo mengine viongozi hao waliyajadili masuala ya usalama, uchumi na biashara.

https://p.dw.com/p/1Bbc0

Ilionekana tokea mapema kabisa kuwa pana kizingiti. Ilikuwa wazi haraka,kwa wachunguzi wa masuala ya Afrika ,wakati Kamishna wa kilimo wa Umoja wa Ulaya Ciolos aliposema hivi karibuni mjini Berlin kwamba anataka kuondolewa mara moja kwa ruzuku zinazoteolwa kwa wakulima wa Ulaya kufidia bidhaa za kilimo kutoka Ulaya zinazouzwa katika nchi za Afrika.

Ludger Schadomsky
Ludger SchadomskyPicha: DW/P. Henriksen

Na kwa kweli hatua zilifuatia haraka za kuzipunguza ruzuku hizo. Lakini pana masharti. Nchi za Afrika zinapaswa kuachilia mbali kudai kufikiwa kwa mkataba wa biashara huru baina yao na Umoja wa Ulaya.Nchi za Afrika na Umoja wa Ulaya zimekuwa zinalizungumzia suala hilo.

Ubia wa kiuchumi udhia kwa Afrika

Tokea mwaka wa 2006 mazungumzo hayo yamekuwa yanafanyika pole pole baina ya Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika, Karibian na Asia juu ya kinachojulikana kama mkataba wa ubia wa kiuchumi,EPA . Lakini hata kwenye mkutano wa kilele wa mjini Brussels hakuna makubaliano yaliyofikiwa.Umoja wa Ulaya unataka mtindo wa nipe nikupe.

Ikiwa nchi za Afrika zinataka kuingia katika soko la Umoja wa Ulaya basi nazo zinapaswa kuiacha wazi milango yao ili kuruhusu bidhaa za aina nyingi kutoka Ulaya kuingia katika masoko ya Afrika. Lakini nchi za Afrika zinalikataa tashi hilo la Umoja wa Ulaya kwa kueleza kwamba nchi hizo haziwezi kushindana na bidhaa kutoka Ulaya zinazowekewa ruzuku kubwa, kama jinsi inavyoweza kushuhudiwa katika biashara ya miguu ya kuku .

Mageuzi ni madhara kwa Afrika

Madhara ya kuleta mageuzi ya soko la Afrika yamebainishwa katika mitaala mingi: kuanguka kwa mapato ya ndani kutokana na kuondolewa kwa ushuru wa maduhuli yaani bidhaa zinazoingizwa kutoka nje na pia kuanguka kwa mapato kutokana na kupungua kwa thamani ya fedha za nchi za Afrika zinapobadilishwa na ili kununua fedha za kigeni.Madhara mengine yapo katika sekta za viwanda na kilimo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kushindana.

Mazingira ya mkutano baina ya viongozi wa Afrika na wa Umoja wa Ulaya yalitibuka mapema kutokana na viongozi wa Umoja wa Ulaya kushikilia kinachoitwa mapatano ya muda juu ya ubia wa kiuchumi-EPA. Mfumo huo ni pingamizi kubwa ya maendeleo na unashindilia msingi wa dhulma-yaani wa kutokuwapo usawa katika uhusiano baina ya nchi za Afrika na Umoja wa Ulaya.

Ikiwa Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika kweli zinataka kuhusiana katika msingi wa usawa kama ambavyo imekuwa inasisitizwa wakati wote, basi pana haja ya kuubadilisha msingi wa mazungumzo juu ya mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi EPA

Nchi za Afrika zina haki ya kupewa uwezo wa kudhibiti taratibu za kuyafungua masoko yao hatua kwa hatua ili ziweze kuisimamia mikakati yao ya maendeleo zenyewe. Msingi wa ushirikiano wa maendeleo unapaswa kuwa wa uwazi na mashauriano. Pande zote mbili zina wajibu wa kutafuta njia za kuleta makubaliano yatakayouridhisha kila upande.

Tamko lililotolewa baada ya mkutano wa kilele wa mjini Brussels linasisitiza manufaa ya haki kwa kila upande.Lakini makubaliano yanayotokana na mashinikizo kwa manufaa ya wauza bidhhaa wa nchi za Ulaya hakika siyo njia sahihi.

Mwandishi:Schadomsky Ludger

Tafsiri;Mtullya Abdu

Mhariri: Yusuf Saumu