1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Je, Mayahudi wana maisha Ulaya?

27 Januari 2020

Miaka 75 baada ya kambi ya Auschwitz kukombolewa, bado Mayahudi barani Ulaya hawajihisi kama wako salama, anasema Rais wa Mabaraza la Viongozi wa Kongamano la Viongozi wa Kiyahudi barani humo, Pinchas Goldscmidt,

https://p.dw.com/p/3Ws05
Pinchas Goldschmidt Oberrabbiner von Moskau
Picha: picture-alliance/K. U. Heinrich

Miaka 75 imepita tangu treni ya kubebea mifugo ilipowasafirisha Jacob na Mariam Schwartz, babu na bibi wa wazazi wangu, kutoka Hungary hadi kambi ya Auschwitz-Birkenau. Huku jua la kiangazi likiwaka, wakiwa na njaa na kiu, na wakiwa wanaogopa na wamechoshwa kwa safari hiyo ya siku tatu, walipelekwa kwenye chumba cha gesi na kuchomwa.

Watu wengine kadhaa kutoka familia ya mama yangu nchini Hungary, wanaume, wanawake na watoto, walikuwa miongoni mwa Mayahudi laki nne wa Hungary waliouawa kwenye kambi hiyo ya Auschwitz.

Mwaka mmoja baadaye, kambi hiyo ya mauaji ilikombolewa na Jeshi Jekundu la Kisovieti, lakini ni manusura wachache tu waliokutikana hapo. Takribani mahabusu wote walikuwa wameuawa ama kupitia vyumba vya gesi, maradhi au kupigwa risasi kwa pamoja.

Nikiwa kama kiongozi wa Kiyahudi, hili si somo la historia tu kwangu. Watu walionizunguka - wale wanaosali kwenye sinagogi langu, wanaokusanyika kwa shughuli za kijamii, wanaosherehekea Bar Mitzvah au wanaomboleza kifo cha mwanafamilia - ni jamaa wa watu kama Jacob na Mariam. Jamii ya Kiyahudi ya Ulaya inaundwa na mauaji ya maangamizi ya Holocaust.

Kuhama Ulaya

Gedenken in Auschwitz zum 75. Jahrestag der Befreiung
Lango la kuingilia kambi ya mauaji ya AuschwitzPicha: picture-alliance/ANP/R. de Waal

Mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, idadi kubwa ya manusura wa mauaji hayo ya maangamizi ilihisi hakukuwa na maisha yaliyobakia kwa Mayahudi barani Ulaya. Wengi wakahamia Palestina kuwa sehemu ya taifa jipya la Kiyahudi, ambako daima Mayahudi wangelipokelewa. Wengine wakahamia mabara ya Amerika, na wachache tu ndio waliobakia Ulaya, waking'ang'ania imani kwamba wangeliweza kuyajenga maisha ya Kiyahudi kwenye bara hili.

Kwa zaidi ya nusu karne, Ulaya yenyewe ilikuwa imegawika baina ya kambi ya mashariki na ya magharibi na huku Pazia la Chuma likiligawa bara hili na jamii yake ya Kiyahudi.

Kwenye mataifa mengi ya Ulaya Magharibi, maisha ya Mayahudi yalipewa mwanga wa matumaini na manusura na wahamiaji wapya; kwa upande wa Ulaya Mashariki, jamii pekee iliyokuwa hai ya Kiyahudi ilikuwa ni nchini Romania, ambako ujuzi wa kiongozi mkuu wa Mayahudi, Moses Rosen, uliwezesha makubaliano na utawala wa kikomunisti na kupata uhuru wa kuabudu na uhuru wa kuhamia kwa jamii yake.

Ambapo uamuzi wa kubakia Ulaya ulikuwa ni wa mtu binafsi kutokana na hali aliyokutana nayo mtu huyo, kwa Mayahudi wengi matumaini ya maisha mema barani humu yalijikita kwenye mifumo na maadili mapya yaliyokuwa yakiendelezwa ili kuhakikisha kesho isiyo vita na chuki dhidi ya Mayahudi.

Ulaya yapaswa kuwa salama

Moshe Ha-Elion
Moshe Ha-Elion, mwenye miaka 95, ni miongoni mwa manusura wa Auschwitz.Picha: DW/P. Kouparanis

Kile kilichokuja baadaye kuwa Umoja wa Ulaya kiliasisiwa kama muungano wa kiuchumi wenye lengo kuu la kukomesha hali ya kudumu ya vita na mashindano baina ya mataifa makubwa yenye nguvu.

Umoja wa Ulaya, kwa mujibu wa Rais wa zamani wa Kamisheni ya Ulaya, Roman Prodi, ulikuwa kutaniko la wachache, ambalo liliwasaidia Mayahudi wa Ulaya kuwa sehemu ya mchakato, na sio wakando, bali raia kamili wa Ulaya.

Hata hivyo, leo hii ukweli ni kwamba mradi huo wa Ulaya haujafanikisha malengo yake yote. Tunafahamu kuwepo kwa chuki dhidi ya Mayahudi kama tunavyojuwa kila siku.

Miaka kumi na tano iliyopita, ugaidi uliikumba Ulaya na hasa Mayahudi wa Ulaya; mashambulizi kwenye nchi nyingi za Ulaya yalifanyika bila kushughulikiwa.

Tangu hapo, chuki dhidi ya Mayahudi zimeshika kasi na sasa zinaongozwa na pande tatu: siasa kali za mrengo wa kulia, siasa kali za mrengo wa kushoto na kupitia siasa kali za kidini. Bahati mbaya, Mayahudi wa Ulaya wanapaswa kujiuliza tena ikiwa bado kuna maisha kwao ndani ya bara hili.