1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Hakuna "muujiza wa Tehran“

11 Juni 2019

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas nchini Iran iliweka wazi kuwa jukumu la Ulaya katika Mashariki ya Kati ni suala zaidi la kiubinadamu

https://p.dw.com/p/3KA8B
Bundesaußenminister Heiko Maas in Teheran
Picha: picture-alliance/AA/Iranian Presidency

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani alienda Tehran mikono mitupu, na akarudi mikono mitupu. Hakukuwa na "muujiza wa Tehran": Makubaliano ya nyuklia hayakuokolewa, wala kanda hiyo haikubadilika mara moja kwa kupunguzwa mvutano. Kwa hali yoyote, hakuna aliyestahili kuwa na matarajio makubwa ya "ziara hii katika eneo la mgogoro", kama alivyoeleza msemaji wa Maas. Upande ambao hasa unaopaswa kupunguza uhasama katika Ghuba ni Marekani – na haikuwa kwenye meza ya mazungumzo.

Kampeni ya Iran ya „"shinikizo kubwa" kama inavyolenga, inaukaba uchumi wa Iran. Mauzo ya mafuta yamepungua, kuna mfumko mkubwa wa bei, na thamani ya sarafu ya nchi hiyo inaporomoka. Shinikizo pia linaongezeka kwa siasa za ndaniza Iran. Matokeo yake: Iran inakaribia mwisho wa "uvumilivu wa kimkakati" ambao imekuwa ikionyesha mpaka sasa. Tehran inaomba msaada thabiti wa kupinga vikwazo vya Marekani – au, viondolewe. Lasivyo, imetishia kuwa kuanzia Julai 7, itaanza kuanza kukiuka ahadi zake chini ya makubaliano ya nyuklia, hasa kuhusiana na urutibishaji wa madini ya urani kupita kiwango kinachoruhusiwa.

Iran | Außenminister Maas und Sarif auf Pressekonferezenz
Maas alikutana pia na mwenzake wa Iran ZarifPicha: Getty Images/AFP/A. Kenare

Lakini mwanadiplomasia huyo mkuu wa Ujerumani hakuweza kufanya chochote zaidi ya kuutaja mfumo wa kufanya biashara barani Ulaya maarufu kama INSTEX kama njia ya kukwepa vikwazo vya kifedha vya Marekani. Ingawa, mpaka sasa, hakuna biashara hata moja iliyofanyika kupitia INSTEX.

Nchi za Ulaya lazima ziunge mkono makubaliano ya nyuklia, na kwa sababu nzuri. Lakini wanaonekana kuwa wanyonge katika kujaribu kuyaweka hai makubaliano hayo kinyume na dhamira ya serikali ya Marekani. Hayawezi kuhakikisha mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara ambayo yaliahidiwa kama Iran itadhibiti silaha zake za nyuklia. Mabenki, na makampuni yanayofanya biashara na Marekani yanahofia kulengwa na mamlaka za kifedha za Marekani.

Huku manowari za kubeba ndege za kivita zikiwa zimetumwa katika eneo la Ghuba pamoja na wanajeshi na ndege za kivita, ni jambo zuri pia kuwa wanadiplomasia wanaelekea katika eneo hilo pia. Hali ni ya hatari sana. Hakuna upande unaotaka vita. Katika hali hii, kutoelewana kunaweza kusababisha janga. Kila mbinu ya mawasiliano ni muhimu sana. Hasa kama Marekani na Saudi Arabia zitashirikiana, kama tu ziara ya Waziri Mkuu wa Japan Shinzo be nchini Tehran, au mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia Mohamed bin Zayed mjini Berlin zote zikiwa ni Jumatano wiki hii.

Mwishowe, hata hivyo, hakuna kukwepa haja ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani. Ulimwengu mzima una maslahi katika mazungumzo haya, na Maas atakuwa amewasilisha ujumbe wao mjini Tehran. Lakini Iran haitokaa kimya kwenye meza ya mazungumzo wakati kisu cha vikwazo kikiwa kimewekwa kwenye koo lake.

/dw/en/opinion-in-tehran-diplomatic-hope-dies-last/a-49131560