MANILLA. Mateka watatu waokolewa nchini Ufilipino.
25 Mei 2005Matangazo
Mateka watatu wa rehani wameokolewa nchini Ufilipino baada ya kuzuiliwa na kundi la watekaji nyara kwa siku moja. Mateka hao waliruka kutoka kwa motokaa iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi na magaidi hao, na wamepelekwa hospitalini kupata matibabu.
Watu watatu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na makombora waliwazuilia wanawake 12 na watoto ndani ya basi la abiria kusini mwa nchi hiyo. Polisi wanashuku watekaji nyara hao, ni magaidi wa kundi la eneo hilo na wala sio wanamgambo wa kiislamu au wa kikomunisti ambao wana ngome zao katika kisiwa cha Mindanao.