MANILA
16 Februari 2005Matangazo
Vikosi vya usalama vya Philippine vimo katika msako mkali kuwatafuta wanamgambo wa Kiislamu wanaowatuhumu kuhusika na mashambulio ya mabomu yaliyotokea juzi siku ya Jumatatu mjini Manila,pamoja na miji mingine miwil, ambapo watu 11 waliuawa na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa.
Kikundi kidogo cha wanamgambo wa Kiislamu cha Abu Sayyaf ambacho kinauhusiano na mtandao wa al Qaeda,kilijigamba kuhusika na miripuko hiyo.Kikundi hicho kimedai kuwa kiliendesha mashambulio hayo kwa lengo la kuiadhibu serikali kutokana kushambuliwa kwa ngome yake kuu kusini-mashariki mwa kisiwa cha Jolo.
Rais wa Philippine Gloria Arroyo amekwishaapa kutumia nguvu za jeshi la nchi hiyo kukitokomeza kikundi hicho.