Manila. Wafilipino waandamana kumtaka rais Arroyo kujiuzulu.
13 Julai 2005Matangazo
Mamia kwa maelfu ya Wafilipino wamejikusanya katika mji mkuu Manila kutoa mbinyo kwa rais Gloria Macapagal Arroyo kujiuzulu kwa madai ya udanganyifu katika uchaguzi mkuu nchini humo.
Polisi na majeshi ya nchi hiyo yako katika hali ya tahadhari na eneo la kibiashara la Makati katika mji mkuu Manila limefungwa kabla ya maandamano hayo kuanza.
Arroyo ameomba radhi kwa kile alichosema ni kuteleza katika maamuzi baada ya kumpigia simu afisa wa tume ya uchaguzi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2004, lakini amekanusha madai hayo ya kufanya udanganyifu.
Amekataa kujiuzulu, akisema kuwa hiyo itasababisha mzozo wa kisiasa katika nchi hiyo.