1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila. Wabunge wa upinzani wataka rais ashitakiwe.

25 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEr0

Wabunge wa vyama vya upinzani nchini Philippines wametoa madai ya kumshtaki rais Gloria Macapagal Arroyo kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Madai hayo yanaelezea madai ya hapo kabla ya vyama vya upinzani kuwa Arroyo alishirikiana na maafisa wa tume ya uchaguzi ili kushinda uchaguzi wa May 2004, pamoja na shutuma kuwa familia yake imepokea hongo kutoka kwa matajiri wa biashara ya kamari ambao hawana leseni.

Wasaidizi wa Arroyo wamejaribu kuzuwia madai hayo katika njia ya kisheria baada ya bunge kukutana kufuatia hotuba inayotarajiwa kutolewa na rais Arroyo kuhusu hali ya taifa leo Jumatatu.

Arroyo amekana kula njama za kuendea kinyume uchaguzi huo na amesema kuwa yuko tayari kupambana na madai hayo ya kumshtaki na kusafisha jina lake.

Pia ametangaza kuwa tume ya kutafuta ukweli itachunguza madai hayo dhidi yake.