1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA. Ufilipino yalalamikia hatua ya nchi za Ulaya ya kujilimbikizia madawa ya homa ya ndege

12 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElW

Waziri wa afya wa Ufilipino Francisco Duque amezilaumu nchi za Ulaya na marekani kwa kujilimbikizia madawa ya ugonjwa wa homa ya ndege na kupuuza hali ya afya ya nchi za ulimwengu wa tatu.

Waziri huyo aliyasema hayo katika mkutano uliohudhuriwa na nchi 11 za Asia mjini Bangkok uliokuwa na lengo la kuanzisha mtandao wa dharura wa nchi hizo wa kukabiliana na hali ya dharura ya maradhi hayo itakapotokea.

Shirika la afya duniani WHO linahofia kwamba virusi vya ugonjwa wa ndege huenda vikavuka mpaka na kuanza kuwaambukiza wanadamu.

Kampuni moja ya madawa ya Uswisi imesema kuwa Ujerumani imeagizia dozi milioni sita za dawa ya homa ya ndege.

Marekani nayo imesema kuwa imefanikiwa kupata kinga ya ugonjwa huo lakini inakabiliwa na kikwazo cha kutengeneza kinga hiyo kwa wingi iwapo ugonjwa huo utasambaa kwa haraka.