MANILA Rais Arroyo ashinikizwa ajiuzulu
14 Julai 2005Matangazo
Maelfu ya raia walifanya maandamano mjini Manila Ufilipino, wakimtaka rais Gloria Arroyo ajiuzulu kwa madai kwamba aliiba kura wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana. Watu wasiopungua elfu 30 walikusanyika katika eneo la biashara la Makati mjini Manila katika maandamano makubwa kabisa tangu kashfa hiyo ilipofichuka.
Rais Arroyo ameomba msamaha kwa kile anachokiita uamuzi usiokubalika wakati alipowasiliana na ofisa wa uchaguzi wakati kura zilipokuwa zikihesabiwa, lakini amepinga madai ya wizi wa kura. Amekataa kujiuzulu akisema hatua hiyo itasababisha mzozo wa kisiasa nchini humo.