Manila. Mtu mmoja akamatwa kwa makosa Phillipines.
6 Novemba 2005Polisi nchini Philippine wanasema kuwa mtu mmoja aliyekamatwa kama kiongozi wa kundi la wapiganaji sio mtu waliekuwa wakimtafuta.
Siku ya Jumamosi , rais wa Philippines Gloria Arroyo alionekana katika televisheni ya taifa akisema kuwa kamanda mkuu wa kundi linaloongozwa na Abu Sayyaf , Radulan Sahiron amekamatwa.
Lakini mkuu wa polisi wa Philippines sasa anasema kuwa mtu waliyemkamata katika msako katika kisiwa cha Basilan kusini mwa nchi hiyo hakuwa Sahiron, bali alikuwa mwanakijiji ambaye alikuwa anafanana na Sahiron.
Amesema kuwa mtuhumiwa huyo atachwa huru bila mashtaka.
Sahiron ni kamanda mkuu wa kundi la Waislamu wenye imani kali la Abu Sayyaf na mmoja kati ya viongozi watuhumiwa waliowateka nyara watu 21, ikiwa ni pamoja na watalii kadha kutoka mataifa ya Ulaya , katika eneo la kitalii nchini Malaysia miaka mitano iliyopita.