1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA: Msiba wa taifa watanagazwa nchini Ufilipino

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn0

Rais Gloria Arroyo wa Ufilipino ametangaza hali ya msiba wa taifa baada ya mporomoko wa matope uliosababishwa na kimbunga cha Durian kuua mamia ya watu.Chama cha misaada cha Msalaba Mwekundu kimesema,vifo vya watu 400 vimethibitishwa na wengine 400 hawajulikani walipo.Kuna hofu kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao itakuwa kubwa zaidi.Takriban watu 30,000 wamepoteza makazi yao na maeneo mengi hayana mawasiliano baada ya nguzo za umeme na simu kuanguka, madaraja kubomoka na njia kuzibwa kwa matope.Kimbunga Durian sasa kimeelekea Bahari ya Kusini ya China na inatarajiwa kuwa kitapunguka nguvu,kabla ya kuwasili Vietnam siku ya Jumatatu.