1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila. Mbunge auwawa kwa bomu.

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1c

Katika mji mkuu wa Phillipines Manila , muasi wa zamani wa kundi la Kiislamu ambaye amekuwa mbunge ameuwawa. Wahab Akbar, ambaye aliunga mkono shambulio la majeshi ya Marekani na Philipines dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu amefariki baada ya bomu kulipuka langoni mwa jengo la bunge.

Tunaamini kuwa bomu hilo liliwekwa katika pikipiki ambayo ilikuwa karibu na gari la mbunge huyo Wahab Akbar.

Dereva wa mbunge huyo pamoja na mfanyakazi wa bunge pia wameuwawa katika mlipuko huo. Bomu hilo lililolipuliwa kutokea mbali kwa chombo maalum liliporomosha paa katika lango hilo la kuingilia katika jengo la bunge na kuharibu magari na kuwajeruhi watu saba wengine ikiwa ni pamoja na wabunge wawili. Rais Gloria Arroyo ametoa amri ya kufanywa uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.