1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA : Majeshi yawekwa katika hali ya tahadhari

12 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4Y

Jeshi la Ufilipino limewaweka wanajeshi 6,000 katika hali ya tahadhari huku kukiwa na hofu ya kuzuka kwa maandamano makubwa ya kupinga serikali yaliopangwa leo hii kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Uhuru wa taifa hilo.

Jeshi la Ufilipino limesema hapo jana kwamba wanamaji wameweka viziuzi vya ukaguzi katika barabara zote kuu zinazoelekea katika mji mkuu ambapo waandamanaji wanatazamiwa kuandamana dhidi ya serikali ya Rais Gloria Arroyo.

Magari yaliosheni wanajeshi kutoka Kikosi cha Operesheni Maalum huko Luzon ya Kaskazini yalianza kuwasili mjini Manila mapema jana asubuhi.Kuwekwa kwa wanajeshi katika hali ya tahadhari kunafuatia wiki ya mvutano wa kisiasa katika taifa hilo la Kusini mashariki mwa Asia lenye idadi ya watu milioni 84 kutokana na madai mapya kwamba Arroyo alifanya udanganyifu katika uchaguzi wa Urais mwaka jana.

Madai hao bado hayakuweza kuthibitishwa na Arroyo amekuwa akipinga wito unaotamka ajiuzulu.