1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila: Maharamia wawaachilia mabaharia wa Ki-Philipino.

17 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG6d

Mabaharia 20 wa Ki-Philipino waliokuwa wametekwa nyara na maharamia katika bahari ya Somalia mwezi March wameachiliwa huru na wapo njiani kuelekea nchini kwao.

Mjumbe maalum wa Philipine huko mashariki ya kati Roy Cimatu amesema kuwa watu hao wameachiliwa wakiwa hawajadhuriwa pahala popote siku ya jumamosi, na haijawekwa wazi ikiwa wamelipia kitu chochote ili waachiliwe.

Ameongeza kuwa yeye hahusiki na makubaliano yoyote kati yao na maharamia hao, lakini anaamini kuwa kumelipwa kiasi fulani cha fedha ili kuachiliwa kwa mabaharia hao.

Kitengo cha wazara ya mambo ya nje cha Philipine kimeripoti kuwa, watu hao walitekwa wakati meli yao ikipakuwa mafuta katika bandari ya kusini mwa Somalia mnamo March 29.

Kitengo hicho kimesema, meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya Arkon yenye makao makuu yake huko Fujaira, umoja wa Falme za kiarabu ambao ndio waliofanya mazungumzo ya kuachiliwa huru kwa mabaharia hao.