Manila: Maandamano ya wananchi dhidi ya Rais wa Philippines
21 Oktoba 2005Matangazo
Maelfu ya waandamaji huko Philippines walijaribu kuandamana hadi kwenye kasri la rais huko Manila. Kulitokea mapambano baina ya waandamaji hao na polisi, huku waandamaji wakirusha mawe. Polisi wanane walijeruhiwa, huku waandalizi wa maandamano hayo wanasema raia watano walijeruhiwa. Waandamaji walikuwa wanataka rais wa nchi hiyo, Bibi Gloria Arroyo,ajiuzulu wakimtuhumu kwamba aliiba kura katika uchaguzi wa mwaka jana. Makundi ya upinzani yamekuwa yakifanya karibu maandamano ya kila siku mabarabarani kujaribu kumuondosha madarakani rais huyo.