1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila. Kimbunga Xangsane kulikumba eneo la Phillipines.

1 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD7G

Kiasi cha watu 200,000 wameondolewa kutoka katika eneo la kati la pwani ya Vietnam wakati kimbunga kinaelekea katika eneo hilo kutoka Phillipines. Kimbunga Xangsane, neno lenye maana ya Tembo, katika lugha ya Kilao, kinatarajiwa kulikumba eneo la pwani ya Vietnam ya kati lenye urefu wa kilometa 1,000 Jumamosi ama mapema leo Jumapili.

Nchini Phillipines , kimbunga hicho kimeuwa kiasi cha watu 61. Watu wengine 69 hawajulikani waliko. Kiasi cha nyumba 15,000 zimeharibiwa. Hicho ni kimbunga kikubwa kabisa kuwahi kulikumba eneo la Manila katika muda wa miongo kadha na kimewaacha mamilioni ya watu bila umeme nchini humo katika kisiwa kikubwa cha Luzon.