1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA: Kimbunga „Utor“ kimefika mwambao wa Ufilipino

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkz

Kimbunga kilichopewa jina la „Utor“ kimefika kwenye pwani ya Ufilipino kikiwa na upepo wenye mwendo wa kilomita 120 kwa saa.Kiasi ya watu 15,000 wamehamishwa kutoka wilaya ya Albay, ukingoni mwa Mlima wa Mayon.Wiki moja iliyopita kimbunga cha „Durian“ kilisababisha mvua kubwa na mafuriko katika eneo hilo la mlima wa volkano. Zaidi ya watu 1,200 walifariki katika mafuriko na matope yaliyoporomoka.