MANILA: Kimbunga kipya kinaelekea Ufilipino
9 Desemba 2006Matangazo
Maafisa nchini Ufilipino wametoa amri ya kuwahamisha kiasi ya watu 15,000,huku kimbunga kikali kikielekea kwenye wilaya ya mashariki ya Albay.Kuna hofu kuwa mvua kubwa huenda zikasababisha mporomoko mpya wa matope,kama ilivyotokea juma lililopita,baada ya eneo hilo kukumbwa na tufani na zaidi ya watu 1,200 kupoteza maisha yao.Ripoti zinasema,kimbunga kipya kinakusanya upepo wa mwendo wa kilomita 120 kwa saa.Mkutano wa kilele wa nchi za Asia ya Kusini-Mashariki na Asia ya Mashariki uliopangwa kufanywa nchini Ufilipino juma lijalo umeahirishwa kwa sababu ya kimbunga hicho.