1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manila. Kimbunga Dorian chaua 300 na kuharibu madaraja.

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnC

Wafanyakazi wa uokozi kutoka upande wa jeshi na raia nchini Phillippines wanapambana na hali baada ya kimbunga kinachojulikana kwa jina la Durian.

Maafisa wanakadiria kuwa watu 300 wameuwawa na idadi kama hiyo hawajulikani waliko katika eneo la jimbo la Bicol, lakini wanatarajia idadi ya watu waliofariki kuongezeka.

Kiasi watu 30,000 hawana mahali pa kuishi na jamii kadha hazina mawasiliano wakati nguzo za umeme pamoja na simu zikiwa zimeharibiwa, madaraja yameharibiwa na barabara kujaa matope na mawe.

Kimbunga Durian kiliingia katika eneo la kusini mwa bahari ya China siku ya Ijumaa baada ya kuwaathiri kiasi cha watu nusu milioni nchini Philippinnes na kinatarajiwa kudhoofika na kuwa kimbunga cha kawaida wakati kitakapokuwa kinaingia katika ardhi ya Vietnam siku ya Jumatatu.