1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA. Arroyo bado ngangari

7 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEde

Maelfu ya waandamanaji wakiongozwa na aliyekuwa rais wa Ufilipino Corazo Aquino wamefanya maandamano ya kumtaka rais Gloria Arroyo wa Ufilipino ajiuzulu.

Maandamano hayo yametokea baada ya upinzani katika bunge kushindwa kupitisha kura ya kutokuwa na imani na rais Gloria Arroyo kwa kuwa na kura chache dhidi ya wabunge wanao muunga mkono rais Arroyo.

Hata hivyo upinzani umesema haukuridhika na matokeo hayo hivyo basi utapekeleka malalamiko yake katika mahakama kuu.