MANAMA:Shirika la kutetea haki za binadamu lasema hakuna uhuru wa kutoa maoni Bahrain
20 Desemba 2006Matangazo
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Bahrain BHRS limetoa ripoti yake inayodai kwamba nchi hiyo inaendelea kukandamiza uhuru wa kutoa maoni.
Ripoti hiyo pia inasema kuna hali ya wasiwasi iliyoanza kujitokeza ambayo inapasa kuangaliwa kwa makini kati ya makundi ya washia na wasunni nchini Bahrain.
Naibu mwenyekiti wa shirika hilo Abdullah al Durazi amesema watapendekeza kupitishwa kwa mswaada unaoharamisha ubaguzi wa kimadhehebu ambao utaweza kupunguza hali hiyo ya mvutano kati ya washia na wasunni.
Hata hivyo bwana Abdullah amesema hali hiyo ya mvutano kati ya madhehebu hayo nchini Bahrain haijafikia kiwango kile kinachoshuhudiwa hivi sasa nchini Iraq ambako mzozo huo unasababisha kuuwawa kwa mamia ya watu.