1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANAMA : Wananchi wa Bahrain wapiga kura ya bunge

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpM

Wananchi wa Bahrain leo wamejitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa taifa kwenye taifa hilo dogo la Ghubahuku kukiwa na mvutano kati ya serikali na upinzani wa madhehebu ya Shia ambao ulisusia uchaguzi hapo mwaka 2002 katika nchi hiyo ya kifalme yenye kuunga mkono mataifa ya magharibi.

Kundi kuu la upinzani limeiambia serikali inayoongozwa na Wasunni kwamba jaribio lolote la kuhujumu uchaguzi huo wa bunge na manispaa litapingwa vikali.

Sheikh Ali Salman wa chama cha taifa cha Al-Wefaq cha Jamii ya Kiislam ambacho kinawakilisha Washia walio wengi nchini humo amesema kundi lake litajuwa iwapo uchaguzi umefanyiwa udanganyifu ikiwa halitoshinda viti 13 kati ya viti 40 vya bunge.

Maafisa wa uchaguzi wamekanusha madai ya kukiukwa kwa taratibu zozote zile za uchaguzi na kusema kwamba wale wanaoutilia mashaka uchaguzi huo bila ya ushashidi watashtakiwa.