1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man City hatihati Champions League

20 Novemba 2012

Michuano ya kombe la vilabu bingwa barani ulaya inarudi tena usiku wa Jumanne (Novemba 20)

https://p.dw.com/p/16miR
Picha: picture-alliance/dpa

Mechi nane za kuwania tiketi ya fainali za mashindano hayo yenye msisimko mkubwa zinachezwa katika makundi E-H. Juventus itakwaana na mabingwa watetezi Chelsea huku Spartak Moscow ikuumana na Barcelona.

Mechi za Jumatano

Michezo mingine ni hapo Jumatano ukiwemo ule kati ya Schalke 04 dhidi ya Ujerumani na Olympiakos ya Ugiriki kwenye kundi B.

Arsenal ya Uingereza itakayomenyana na Montpellier ya Ufaransa katika uwanja wa Emirates wakati AC Milan aya Iatalia ni dhidi ya Anderlecht ya Ubeligiji mchezo wa kundi C.

Arsenal itaingia uwanjani bila mshambuliaji wake Theo Walcott ambaye alijeruhiwa begani katika mechezo uliopita dhidi ya timu hiyo na vijana wa kaskazini ya mji wa London Tottenham Hotspur ambao matokeo yalikuwa ni ushundi kwa Arsenal wa bao 5-2.

Arsenal wakiwa uwanjani
Arsenal wakiwa uwanjani na BarcelonaPicha: picture-alliance/dpa

Mtihani kwa Manchester City

Kwa msimu wa pili mfululizo klabu ya Manchester City ya Uingereza inakabiliwa na kibarua kizito na wasi wasi wa kuyaaga mashindano ya Champions League, katika hatua hii ya makundi.

Kunusurika pekee kwa vijana hao wanaoonekana kushindwa kuwika kabisa katika ligi hiyo ni kuifunga miamba ya Uhispania Real Madrid katika mchezo wa Jumatano, Novemba 21.

Manchester City ambao ni mabingwa wa Ligi ya soka ya Uingereza wameonyesha kiwango duni kabisa katika Champions League kiasi wao ndio wanaofunga mkia kwenye kundi lao D baada ya kupata pointi 2 pekee katika mechi nne walizocheza.

Mshambuliaji wa klabu hiyo Carlos Tevez amesema "tumeanza kucheza mashindano haya mwaka uliopita tu, hivyo tunahitaji uvumilivu kidogo. Tunajua itakuwa ngumu lakini ni lazima kuendelea na mapambano hadi mwisho"

Borussia Dortmund katika moja ya mechi zake
Borussia Dortmund katika moja ya mechi zakePicha: Reuters

Real Madrid inaweza kusonga mbele zaidi katika ligi hiyo kama itaichapa Man City katika mchezo wao wa Jumatano (Tarehe 21 Novemba) katika uwanja wa Etihad.

Real iko pointi moja nyuma ya kiongozi wa kundi lake mabingwa wa Ligi ya Soka ya Ujerumani, Bundesliga, Borussia Dortmund ambayo mchezo ujao itacheza na Ajax Amsteradam ya Uholanzi.

Mwandishi: Stumai George/PDA/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman