SiasaSudan
Mamlaka Sudan yawalenga viongozi wa chama cha Kiislamu
1 Agosti 2023Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa nyaraka zilizoonekana na shirika la habari la Reuters. Nyaraka hizo zilizotolewa na mkoa wa Kassala zinataka maafisa wawakamata Ahmed Haroun, Ali Osman Mohamed Taha na watu wengine watatu ambao walikuwa maafisa waandamizi katika utawala wa miongo mitatu wa Omar al-Bashir.
Vita nchini Sudan vyaonekana kama jaribio la kuibuka kwa udikteta
Wapiganaji wa RSF, wanasiasa na baadhi ya wachambuzi wanasema kwamba vita vya Sudan vilivyodumu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa ni jaribio la kuibuka tena kwa utawala wa kidikteta wa al-Bashir.