Mamilioni ya Waislam wanaanza ibada ya Hajj Makka
9 Agosti 2019Hajj, mojawapo ya mkusanyiko mkubwa kabisa wa watu ulimwenguni ni nguzo ya mwisho kati ya nguzo tano za dini ya kiislam na inabidi itekelezwe na kila muislam mwenye uwezo angalao mara moja katika maisha yake.
Hajj ni mchanganyiko wa ibada zinazotekelezwa kwa muda wa siku tano katika mji mtukufu wa Makka na maeneo ya karibu, magharibi mwa Saudi Arabia.
"Juhudi zote zinafanywa na tuna fahari kuwahudumia wageni wa Mungu" anasema msemaji wa vikosi vya usalama Bassam Attia.
Jumla ya waumini milioni mbili na nusu, wengi wao kutoka nchi za nje wanatekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiiislam mwaka huu-kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Hatem ben Hassan Qadi, viza zaidi ya milioni moja na laki nane zimetolewa kupitia mtandao bila ya watu kulazimika kwenda ubalozoini."Ni ufanisi mkubwaa huo" anasema.
Hisia za aina pekee kwa mahujaj
"Tunajisikia tumetakasika" tunaapotekeleza Hijja na kuonana na watu kutoka kila pembe ya dunia" anasema kwa furaha Mohammed Jaaffar, hujaj wa miaka 40 kutoka Misri.
Ni hisia isiyokuwa na mfano, haisimuliki bila ya kuiishi" anasema bibi mmoja wa miaka 50 aliyekuja kwa mara ya kwanza kuhiji Makka."Ni fursa adhimu" anasema bibi mwengine aliyefuatana nae.
Katika mji wa Makka, unaokutikana bondeni na jangwani, ndiko inakokutikana Qaaba-kati kati ya Misikiti mtukufu wa Makka.Waislam wa ulimwengu mzima wanaelekea Qaaba wanaposali mara tano kwa siku. Mahujaj wanabidi waizunguke Qaaba mara saba-au Tawaf.
Hajj ni mchanganyiko wa ibada zinazofanyika katika msikiti mtukufu wa Makka na maeneo ya karibu na hapo.
Mahema ya rangi nyeupe yaenea Mina
Hii leo mahujaj wanashiriki katika sala ya ijumaa katika msikiti mkuu wa Makka-Masjidi Haram. Baadae milolongo ya waumini wataelekea Mina, karibu na Makka kwa mguu au kwa mabasi. Mina mji wa bondeni uliozungukwa na milima ya mawe hugeuka kambi kubwa ya mahema meupe kila mwaka wakati kama huu. Mwaka huu mahema laki tatu na nusu yamewekwa ili kuwapokea mahujaj.
Kesho ijumamosi waumini watapanda mlima Arafat unaojulikana kama Mlima wa Rehma kwaajili ya kuomba duwa na kutubia kabla ya kurejea Mina kwaajili ya ibada ya kumpiga mawe shetani au Jamarat. Ibada hiyo ndio mwanzo wa siku kuu ya iddi el Adha ambayo itasherehekewa jumapili inayokuja. Baadae mahujaj wanabidi warejee katika msikiti mkuu wa Makka kuizunguka mara saba Qaaba, ili kuwaga.
MwandishiHamidou Oummilkheir/dpa/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo