1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mamia ya watu wahamishwa kutoka mpaka wa Ukraine

11 Mei 2024

Mamia ya watu wamehamishwa kutoka maeneo ya karibu na mpaka wa Urusi katika mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine, siku moja baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya kushtukiza ya ardhini

https://p.dw.com/p/4fjv4
Uharibifu uliosababishwa na shambulizi la Urusi katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine mnamo Mei 10,2024
Shambulizi la Urusi katika mji wa Kharkiv nchini UkrainePicha: Vyacheslav Madiyevskyy/Ukrinform/picture alliance/abaca

Katika ujumbe aliouandika kwenye mitandao ya kijamii, gavana wa Kharkiv Oleg Synegubov, amesema takriban watu 1,775 wamehamishwa. Pia ameripoti kuhusu shambulio la mizinga na silaha nyingine za Urusi dhidi ya makazi 30 katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Zelensky athibitisha kuweko kwa mapigano makali Kharkiv

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kuwa mapigano makali yanaendelea katika eneo hilo la Kharkiv na kwamba ni lazima wavuruge operesheni za uchokozi za Urusi na kuchukuwa udhibiti wa hali hiyo.

Watu watatu wauawa kutokana na shambulizi la Ukraine

Huku hayo yakijiri, Gavana wa eneo la Luhansk linalokaliwa na Urusi mashariki mwa Ukraine Leonid Pasechnik, amesema leo kuwa watu watatu wameuawa kutokana na shambulizi la Ukraine kwenye ghala la mafuta.