1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya wafungwa waachiwa huru nchini Yemen

Admin.WagnerD30 Septemba 2019

Waasi wa Houthi wamewaachia huru mamia ya watu waliokuwa wanawashikilia kama wafungwa kwenye maeneo wanayoyadhibiti, hatua ambayo imeleta tumaini la kurejea mazungumzo ya amani kati ya pande zinazopigana nchini Yemen. 

https://p.dw.com/p/3QVuq
Jemen Sanaa | Huthi Rebellen lassen mehrere hundert Insassen frei
Furaha ya kuwa huruPicha: Reuters/K. Abdullah

Mapema siku ya Jumatatu watu 290 waliokuwa wakishiliwa na waasi wa Houthi waliachiwa huru kutoka jela moja  iliyopo mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Ndugu na jamaa za wale walioachiwa walikuwepo mara zoezi hilo lilipofanyika na Turki Alsaadi mmoja ya watu waliokuwa wakishiliwa gerezani amesema "Namshukuru mungu kwa tunu hii ya kuachiwa huru na tunashukuru mchakato huu wa kiutu wa kuwaachia huru wafungwa na tunazitolea wito pande zote kufanya kazi pamoja kutatua suala la wafungwa chini ya misingi ya kiutu ili kumaliza mateso kwa familia zao"

Wale waliochiwa leo walikamatwa kwenye  matukio ya uvamizi yaliyoendeshwa na waasi wa Houthi tangu mwaka 2014 wakati walipoudhibiti mji mkuu Sanaa na maeneo mengine ya kaskazini ya Yemen.

Waasi wa Houthi wataka hatua sawa kutoka kwa mahasimu wao

Jemen Kämpfer der Houthi-Rebellen
Wapiganaji wa KihouthiPicha: picture-alliance/AP Photo/H. Mohammed

Abdul Qader Al-Mortada, mkuu wa kamati ya kitaifa ya waasi wa Houthi inayoshughulikia masuala ya wafungwa amesema jumla ya wafungwa 350 wataachiwa huru katika awamu ya kwanza.

"Tumewasilisha kwa Umoja wa Mataifa mpango wetu wa kuwachia wafungwa 350 waliorodheshwa kwenye makubaliano ya Sweden na tumeuomba Umoja wa Mataifa kuushinikiza upande wa wachokozi kuchukua hatua kama hiyo ya kuwachia wafungwa" amesema Al-Mortada

Kamati ya msalama mwekundu ndiyo imefanikisha zoezi la kuachiwa wafungwa baada ya kupokea maombi kutoka waasi wa Houthi.

Mkuu wa kamati hiyo nchini Yemen ameelezea matumaini yake kwamba tukio la leo linaweza kufungua milango ya kuachiwa wafungwa zaidi ili kurejesha furaha kwa familia zinazongojea kujiumuika tena na wapendwa wao.

Umoja wa Mataifa wakaribisha hatua hiyo

Humanitäre Krise in Jemen
Picha: picture-alliance/M. Hamoud

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Martin Griffiths, ameikaribisha hatua hiyo ya leo na amezitolea wito pande zote kuhakikisha wafungwa walioachiwa wanarejea salama makwao.

Kadhalika amezikaribisha pande zinazopigana kurejea kwenye meza ya mazunguzmo katika kipindi kifupi kijacho kuendeleza majadiliano yalaliyoanza nchini Sweden mnamo mwaka uliopita ambapo pande hizo zilitia saini makubaliano yaliyojumuisha kauchiwa hruu kwa wafungwa 15,000.

Muungano wa kijeshi unaongozwa na Saudi Arabia ulijiingiza kwenye mzozo wa Yemen mwaka 2015 na tangu wakati huo umekuwa ukipambana na waasi wa Houthi kujaribu kuirejesha madarakani seirkali ya rais Abdu Rabbo Mansour Hadi.

Mapigano kwenye taifa hilo masikini zaidi la kiarabu yamesababisha mzozo mkubwa wa kibinaadamu ambao umewaacha mamilioni ya watu bila chakula wala huduma za afya.