Mamia wawakumbuka wasoshalisti wakijerumani Berlin
13 Januari 2008Matangazo
BERLIN:
Watu maelfu kadhaa wamekusanyika leo mjini Berlin kuwakumbuka washoshalisti wawili wa kijerumani-Rosa Luxemburg na Karl Liebkneicht, waliouliwa miaka 89 iliopita.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria ni mwenyekiti wa chama cha mrengo wa kushoto- Lothar Bisky na kiongozi wa kundi la wabunge wa chama hicho-Gregor Gysi.Luxemberg na Liebknecht waliuliwa na makamando wa mrengo wa kulia januari 15 mwaka wa 1919.