Mamia wapoteza kazi baada ya jeshi kufungia vituo vya habari
29 Mei 2024Matangazo
Hayo yameelezwa na muungano wa vyombo vya habari ambao unajiandaa kuitisha mgomo wa nchi nzima.
Muungano huo siku ya Jumatatu ulitishia kuanzisha mgomo wa nchi nzima usiokuwa na kikomo baada ya mamlaka nchini Guinea kufuta leseni za uendeshaji wa shughuli za vituo sita vya habari wakati nchi hiyo ikiwa inakabiliwa na wasiwasi wa kijamii na mazingira mabaya ya kisiasa.
Muungano huo wa SPPG umevitaka vyama vyote vya wafanyakazi kupitia barua iliyoonekana leo na AFP, kuunga mkono mgomo huo.
Mamlaka zimesema kufungiwa vituo hivyo vya habari kumetokana na vyombo hivyo kushindwa kutekeleza maagizo kuhusu maudhui wanayorusha hewani.