Wafanyabiashara wa Kampala wamekusanyika katikati mwa mji kupinga kile wanachokitaja kuwa kunyanyaswa na raia wa China wanaofanya biashara za rejareja na kuuza bidhaa sawa na zao kwa bei ya chini.
Mgomo huo umeungwa mkono na viongozi wa mji wakiwemo meya Erias Lukwago na mbunge wa eneo hilo Muhamad Nsereko ambaye amekamatwa na kuzuiliwa kwa muda na polisi kwa madai ya kuwachochea wafanyabiashara waafrika.