1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Historia

Malkia Muhumuza - aliyepambana na ukoloni

Yusra Buwayhid
25 Julai 2018

Kutana na Malkia Muhumuza, mke wa mfalme Kigeli wa Rwanda anayekumbukwa kwa kupambana na mfumo dume na ukoloni.

https://p.dw.com/p/324Ae

Takriban miaka 100 iliyopita nchini Uganda, mwanamke mmoja alisimama kidete dhidi ya mfumo dume na ukoloni. Alikuwa kiongozi wa kiroho, kiongozi wa kijeshi na mpiganiaji wa haki za kijamii.

Alipoishi: Siku hasa aliyozaliwa malkia Muhumuza haijulikani kwa hakika lakini inaaminiwa aliishi kutoka karne ya 18 hadi ya 19. Alikuwa mke wa Mfalme Kigeli wa IV. Mume wake alipofariki mwaka 1895, na mwanawe wa kiume kunyimwa ufalme, aliasi dhidi ya uongozi wa kikoloni. Alihamia Uganda, na alikamatwa mara kadhaa na vikosi vya wakoloni wa Kiingereza na kufungwa katika gereza la Mengo, alipofariki dunia mnamo mwaka 1945. Muhumusi hakupata fursa ya kurudi kwao alipozaliwa.

Alijulikana zaidi kwa: uwezo mkubwa wa kiroho inayoaminiwa na baadhi kuwa ameurithi kutoka kwa malkia maarufu wa Kiafrika - Nyabingi. Muhumuza alielezewa na wakoloni wa Kiingereza "kama mtu wa ajabu." Wengi wa wafuasi wake hawakumtambua kwa sura kwavile daima alikuwa akijificha ndani ya kapu.

African Roots Muhumusa
Picha: Comic Republic

Aliheshimiwa kwa: kupambana na wakoloni wa aina tatu tofauti - Wajerumani, Waingereza na Wabelgiji, akipinga kanuni zinazokandamiza haki za wanawake ndani ya jamii.

Utata: Baadhi ya wafuasi wake wakiamini kwamba Muhumuza mwenyewe ndiye Malkia Nyabingi. Wengine wanaamini kwamba roho ya Malkia Nyabingi ameipokea Muhumusa alipozaliwa, au pengine ana nguvu zisizo za kawaida za huyo Malkia Nyabingi, ambaye nae pia alitokea Rwanda na aliishi karne kadhaa kabla ya kuzaliwa Muhumusa. Kwa bahati mbaya, historia ya Muhumusa haikurekodiwa kikamilifu kutokana na mfumo dume uliokuwa umetawala jamii ya Rwanda wakati huo pamoja na utawala wa kikoloni.

Anakumbukwa kwa: Kuhamasisha vuguvugu la kupinga ukoloni nchini Rwanda na Uganda. Leo hii, wafuasi wake wanamtazama kama mtu wa kuingwa na mwakilishi wa kuheshimika wa kupinga kanuni zinazokandamiza baadhi ya makundi ndani ya jamii. Anakumbukwa zaidi miongoni mwa waumini wa vuguvugu la Urastafari.

Asili ya Afrika :Malkia Muhumuza

Jane Ayeko-Kümmeth na Philipp Sandner wamechangia kuandika makala hii. Ni sehemu ya makala maalum za mfululizo wa "Asili ya Afrika", ushirikiano kati ya shirika la DW na taasisi ya Gerda Henkel.


Tafsiri: Yusra Buwayhid
Mhariri: Garce Patricia Kabogo