Malkia Elizabeth ziarani Irland Kaskazini
27 Juni 2012Hatua hii imeonyesha kuleta hali ya maridhiano tangu kufanyika kwa ghasia za IRA mwaka wa 1979 zilizosababisha maelfu ya wanajeshi na raia kuuwawa akiwemo binamu wa Malkia Elizabeth.
Mkutano huo kati ya Malkia Elizabeth na McGuinness, ambaye kwa sasa ni naibu waziri wa kwanza wa Ireland kaskazini umekuja miaka 14 baada ya jeshi la IRA kumaliza vita vyake dhidi ya utawala wa Uingereza katika mkoa huo. Hii hata hivyo imeonekana moja kwa moja kuwa ni hatua muhimu katika mchakato mzima wa amani.
Malkia Elizabeth alikutana na naibu waziri huyo wa kwanza wa Ireland kaskazini McGuinness, Peter Robinson ambaye ni waziri wa kwanza anayepigania muungano wa Ireland mbili na rais wa Irish Michael D.Higgins kwa muda wa dakika kumi ndani ya chumba kimoja ambapo nje kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi. McGuinness alisalimiana kwa kupeyana mkono na malkia kwa mara ya pili baada ya kutoka katika mkutano wao wa faragha. Kwa mara hii ya pili walisalimiana mbele ya kamera za vyombo vya habari lakini Mc Guiness hakuinamisa kichwa chake chini kama ilivyo desturi ya wageni wengine wanapokutana na malkia wa Uingereza.
Vazi la Malkia lililokuwa la rangi ya kijani kibichi lilionekana kuoana na rangi ya taifa la Ireland. Kiongozi huyo wa zamani wa IRA Martin McGuinness alimtakia kheri Malkia katika ziara yake ya siku mbili kwenye kisiwa cha Ireland Kaskazini.
Hata hivyo kumekuwa na upinzani tofauti juu ya dalili ya maelewano kutoka kwa wapinzani wa jeshi la Irish na kutoka kwa waathiriwa wa ghasia za IRA. Lakini wanasiasa wengi wa Ireland kaskazini wanasema wameuunga mkono mkutano huo wa kwanza kati ya Malikia Elizabeth na kiongozi wa zamani wa IRA McGuinness.
Akizungumza na shirika la utanagazaji la BBC, aliyekuwa Waziri wa Uingereza anayehusika na mambo ya Ireland kaskazini, kuanzia mwaka wa 2001 na 2002 John Reid amesema tukio la leo ni tukio kubwa mno.
Mwandishi: Amina Abubakar/RTRE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman