Mali yaanzisha uchunguzi dhidi ya washukiwa wa ugaidi
29 Novemba 2023Matangazo
Wanaochunguzwa ni pamoja na Iyag Ag Ghaly, kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Tuareg na kiongozi wa muungano wa Kiislamu na Waislamu unaohusishwa na kundi la al-Qaeda, na mhubiri wa msimamo mkali kutoka kabila la Fulani Amadou Koufa, ambaye ni mwanachama wa kundi hilo.
Pia kwenye orodha hiyo, ni viongozi sita wa Tuareg wanachama wa muungano wa makundi ya wapiganaji ambao hivi karibuni ulianzisha upya uasi dhidi ya taifa, licha ya kusaini muafaka wa amani mwaka wa 2015 mjini Algiers.
Ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali imesema uchunguzi huo ulianzishwa sio tu dhidi ya viongozi wa kigaidi bali pia wanachama waliosaini makubaliano ya amani ya mwaka wa 2015 na wamejiunga na ugaidi.