1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Mali, Niger na Burkina Faso zakusudua kuunda shirikisho

2 Desemba 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yanayotawaliwa kijeshi ya Burkina Faso, Mali na Niger wamependekeza kuunda shirikisho kama sehemu ya lengo la muda mrefu la kuunganisha mataifa jirani ya Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4Zhfg
Mali, Niger na Burkina zakusudua kuunda shirikisho
Mali, Niger na Burkina zakusudua kuunda shirikishoPicha: AFP

Katika mkutano wao huo kumefanyika makubaliano, chini ya msingi wa kile walichokiita "Muungano wa Nchi za Sahel", wakiwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa karibu wa kiuchumi na usaidizi wa ulinzi wa pande zote ikiwa kuna kitisho kwa mmoja wa nchi mwanachama.

Katika taarifa yao ya pamoja kufuatia mkutano wa siku mbili uliofanyika katika mji mkuu wa Mali, Bamako, mawaziri hao wa mambo ya nje walizungumzia uwezokano mkubwa wa amani, utulivu, umadhubuti wa kidiplomasia na maendeleo ya kiuchumi ili kutoa fursa ya kupatikana kwa  uimara wa kisiasa katika mataifa yao.

Mali na Burkina Faso, zinazotawaliwa na viongozi wa kijeshi ambao walichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2020 na 2022. Na Niger kwa upande wao maafisa wa kijeshi waliingia madarakani Julai kwa kumundoa Rais Mohamed Bazoum.