Muungano wa upinzani wa Lamuka nchini DRC unashinikiza kujiuzulu kwa wabunge wa kitaifa ambao wanapokea mshahara wa dola za Marekani 21,000 katika nchi ambayo raia wanakabiliwa na umaskini mkubwa. Mratibu wa Lamuka, Martin Fayulu, anaelezea hali hiyo kama ufisadi. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu kutoka Kinshasa Jean Noël Ba-Mweze.