MALABO : Mugabe afanya ziara ya ghafla E. Guinea
3 Machi 2007Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili katika mji mkuu huo wa kiuchumi wa Equatorial Guinea hapo jana katika ziara ambayo haikutangazwa.
Alipokelewa kwenye uwanja wa ndege na rais mwenzake wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema mwanzoni mwa ziara yake huko Bata ambayo duru zilizo karibu na serikali zimesema kuwa ni ya kibinafsi.
Viongozi hao wawili wanapanga kuwa na mazungumzo wakati wa ziara hiyo ya Mugabe inayomalizika hapo kesho usiku.
Katika ziara iliopigiwa debe mno hapo mwezi wa Novemba mwaka 2004 nchini Equatorial Guinea Mugabe alitangazwa kuwa muokozi mjini Harare na Malabo kwa kuzima njama ya kumpinduwa Rais Nguema.
Kiongozi wa njama hiyo Simon Mann raia wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha miaka minne nchini Zimbabwe lakini serikali ya Equatorial Guinea inapigania apelekwe nchini humo.